Katika baadhi ya hadithi, imeandikwa kwamba Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atatawala kwa uadilifu kiasi kwamba wakaazi wa mbingu na ardhi watakuwa radhi naye, na popote atakapokwenda duniani, Allah Ta‘ala atasababisha wema na baraka kushinda. Uadilifu wake utawazunguka watu wote na atawatawala kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).
Kwa ajili ya uadilifu wake, atakapomuelekeza mtu kutangaza, “Mwenye haja aje kwangu,” atakuja mtu mmoja tu (kama vile mahitaji ya watu wengine wote yatakuwa yametimizwa kutokana na utawala wake wa haki).
Abu Sa’eed Khudri (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba siku moja, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliwahutubia Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) akisema, “Nakupa bashara njema ya Mahdi (Radhiyallahu ‘anhu) akija kwenye ummah huu (kabla ya Qiyaamah)! Atatumwa kwa ummah huu katika wakati ambapo ikhtilafu baina ya ummah zitakuwa nyingi na matetemeko ya ardhi yatashuhudiwa duniani. Atatawala kwa namna ambayo dunia itajawa na uadilifu, kama vile hapo awali ilivyokuwa imejaa na uonevu na dhuluma. Wakaao mbinguni na wakaao duniani watakuwa radhi naye. Atagawanya mali kwa usahihi.”
Kisha Swahaabi mmoja (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)! Nini maana ya Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atagawanya mali kwa usahihi?” Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu: “Ina maana kwamba atagawanya mali kwa usawa na uadilifu baina ya watu.”
Kisha Rasulullah (Sallallahu alihi wasalllam) akaendelea, “Wakati huo, Allah Ta’ala atajaza nyoyo za umma wa Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam) kuridhika na furaha. Utawala wa uadilifu wa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) utawazunguka watu, mpaka watu watapata baraka kubwa kupitia kwake, kiasi kwamba mtu atawahutubia watu akisema, ‘Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye haja ya mali?’ Kutoka kwa watu wote, ni mtu mmoja tu atakayesimama na kusema, ‘Mimi niko na mahitaji ya mali!’
“Mtu huyo atamwambia, ‘Nenda kwa mweka hazina na umwambie, ‘Mahdi amekupa maagizo ya kunipa mali.’ Atakapokuja kwa mweka hazina, mtunza hazina atamwambia, ‘Chukua mali kwa mikono yako miwili, kadiri unavyotaka!’ Mtu huyo atachukua mali na mikono yote miwili akizikusanya mbele yake.
“Wakati huo, mtu huyo atajuta na kusema, ‘Mimi nilikuwa mwenye kutamani sana mali zaidi katika umma wa Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam)! Je, hayo yaliyowatosheleza hayawezi kunitosheleza?’ Akisema hivi, anarudisha mali. Lakini, mali atakayotaka kuirejesha kwa Mahdi (Radhiyallahu ‘anhu) haitakubaliwa kutoka kwake, na ataambiwa, ‘Tunachotoa haturudishi.’
“Sharti hii ya baraka itaendelea kuwepo katika muda wote wa Mahdi ambao ni miaka saba, minane au tisa.” (Majma’uz Zawaa’id #12393)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu