Abdullah ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu anhu) Akisoma Qur-aan Majeed kwa sauti mbele ya Waquraishi

Abdullah ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu anhu) alikuwa mtu wa kwanza kusoma Qur-aan Majeed kwa sauti huko Makka Mukarramah kabla ya Maquraishi baada ya kusilimu.

Siku moja, Maswahabah (Radhiya Allaahu anhum) walikusanyika na kusema: “Wallahi, Maquraish hawajawahi kumsikia mtu yeyote akisoma Qur-aan kwa sauti mbele yao, basi ni mtu gani kati yetu aliye tayari kwenda kusoma Qur-aan kwa sauti mbele yao?”

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Nitakwenda na kuwasomea Qur-aan kwa sauti. Maswahaabah (Radhiya Allaahu anhum) wakajibu: “Tunahofia maisha yako! Tunataka mtu wakuwatangulie na kuwasomea Qur-aan kwa sauti mtu ambaye ana ukoo madhubuti wa kumlinda na watu ikiwa watataka kumdhuru.” Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu akisema, “Niache niende, kwa hakika Mwenyezi Mungu atailinda maisha yangu!”

Siku iliyofuata wakati wa alfajiri, Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliondoka na kufika Maqaam-ul-Ebrahim. Wakati huo, Maquraishi walikuwa wameketi kwenye mikusanyiko yao karibu. Alisimama karibu na Maqaam-ul-Ebrahim, na akaanza kusoma Qur-aan Majeed kwa sauti. Kwanza alisoma Bismillah, na kisha akaanza kusoma Surah Rahman.

Maquraishi walisikiliza kisomo chake kwa makini, na kisha wakaanza kuulizana wao kwa wao, “Ibnu Umm-Abd (wakimanisha Abdullah bin Mas’uud) anasoma nini?” Baadhi yao wakajibu: “Anasoma baadhi ya aya alizowaletea Muhammad. Hapo hapo wakasimama na kuanza kumpiga usoni. Lakini yeye akaendelea kusoma Qur-aan Majeed kwa kadiri aliyoweza kusoma mbele yao.

Baada ya kila kitu kukamilika, Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alirejea kwa masahaba zake katika hali ya kuwa uso wake ulijeruhiwa kutokana na kipigo hicho. Walipomwona katika hali hiyo, masahaba zake wakamwambia: “Tulikuwa tunakuhofia! Akajibu, “Maadui wa Allah Ta’ala si wa maana mbele yangu sasa kuliko hata hapo awali (tukio hili lilitokea yaani Sijali jinsi wanavyonitazama – bali bado nitaendelea kusoma Qur-aan Majeed mbele yao). Ukitaka niende kuwasomea Qur-aan tena mbele yao, basi mimi niko tayari kwenda kesho tena kufanya hivyo.” Wenzake wakamwambia, “Hii inatosha! Tulitaka mtu awasikilizishe kisomo kizuri, na wewe umekamilisha hili kwa kuwafanya wasikie, lakini kwa bahati mbaya, wao hawapendi kusikia. (Usdul Ghabah 3/381)

About admin

Check Also

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Akisifu Kisomo cha Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahi kusimulia tukio lifuatalo: Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akiongea na …