عن حسين بن علي بن أبي طالب قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: البخيل الذي من ذكرت عنده فلم يصل علي (سنن الترمذي، الرقم: 3546، وقال هذا حديث حسن صحيح غريب)
Sayyidina Husain (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “bakhili wa kweli ni yule ambaye jina langu linatajwa mbele yake, lakini hanitumii salamu.”
Dua ya Malaika
Imepokewa kwamba mtu anaposimama kwenye kaburi la
Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na akasoma Aayah ifuatayo:
إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
Na baada ya hapo akimtumia salaa na salaam ifuatayo mara sabini.
صَلّٰى اللهُ عَلَيْكَ يَا مُحَمَّدْ
Basi Malaika husema: “Neema za Allah Ta’ala ziwe juu yako pia”, na Allah Ta’ala humtimizia kila haja yake.
Mullah Ali Qaari (rahimahullah) ana maoni kwamba badala ya kusema ‘Ya Muhammad’, mtu atasema ‘Ya Rasulallah’ itakuwa bora zaidi. ́Allaamah Qastallaani (rahimahullah) amepokea maoni kama hayo kutoka kwa Shaikh Zainud-deen Maraaghi (rahimahullah) na wengine pia.
Sababu yake ni kwamba tumekatazwa kumwita Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa jina lake. Lakini, kama ndani ya Hadith ilinukuliwa neno ‘Ya Muhammad’, basi hili linapaswa kutiliwa muhimu na halibaki kukatazwa.
Sheikh Moulana Muhammad Zakariyya (rahimahullah) ametaja:
Mimi Binafsi nahisi kwamba mgeni katika kaburi la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) anapaswa katika kila ziara, asome mara sabini yafuatayo kwa unyenyekevu kamili:
اَلصَّلَاةُ وَالسَّلَامُ عَلَيْكَ يَا رَسُوْلَ الله