Heshima Ya Umar (radhiya allaahu ‘anhu) kwa Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu)

Umar (radhiya allaahu ‘anhu) siku zote alitambua nafasi ya juu na ukubwa wa Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) na hakujiona kuwa sawa na Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu).

Wakati mmoja, kundi la watu lilimsifu Umar (radhiya allaahu ‘anhu) wakisema, “Wallahi! Hatukuwahi kumuona mtu anayetoa haki, msema kweli na ni mkali zaidi juu ya wanafiki kuliko wewe, ewe Ameer-ul-Mu’mineen! Baada ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), wewe ni mtu mkubwa (wa ummah huu)!”

Aliposikia hivyo, ‘Auf bin Maalik (radhiya allaahu ‘anhu) aliwapinga watu waliotaja maneno haya, “Nyinyi watu hamjasema ukweli! Wallahi nimemuona mtu mwingine ambaye kwa hakika ni mtu mkubwa zaidi baada ya Mtume (sallallahu’alaihi wasallam)!”

Watu walipomuuliza ‘Auf (radhiya allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa anamzungumzia nani, alijibu: “Ninamzungumzia Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) (kwani yeye ndiye mtu mkubwa zaidi wa umma huu baada ya Rasulullah (sallallahu’alaihi wasallam) na Manabii)).

Umar (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akasema, “Wallahi! Auf (radhiya allaahu ‘anhu) amesema ukweli na nyinyi watu hamjasema ukweli! Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa na harufu nzuri zaidi kuliko miski nikiwa bado nimepotea na ni mpotovu zaidi kuliko ngamia wa familia yangu (yaani Umar (radhiya allaahu ‘anhu) aliitaja hii akimaanisha kipindi cha kabla ya kusilimu, na wakati huo, Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) tayari alikuwa na Imaan na alikuwa mtu bora katika Dini). (Manaaqib Umar bin Khattaab libnil Jowzi pg. 141)

About admin

Check Also

Talhah (Radhiyallahu ‘anhu) katika Vita vya Uhud

Kuhusiana na uvumilivu wa Talha (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika Vita vya Uhud, Sa’d bin Abi …