Tahadhari katika Mali Za Umma

Tahadhari ambayo Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa nao wakati wa kushughulika na mali ya umma kwa hakika ilikuwa mithali mkubwa.

Wakati mmoja, miski flani na ambergris (aina ya manukato flani) zilifika kutoka Bahrain. Kwa vile ilikuwa ni mali ya umma, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema, “Wallahi! Natamani nimtafute mtu ambaye ni mjuzi wa kupima uzito ili aweze kunipimia manukato haya, aniwezeshe kugawa kwa usawa baina ya Waislamu.”

Kusikia hivyo, mke wake mheshimiwa, ‘Aatikah binti Zaid (Radhiya Allaahu ‘anha), akajitolea kutimiza huduma hii akisema, “mimi ni mtaalam wa kupima mizani. Zilete nitakupimia.” lakini, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa ombi lake.

Kisha akamuuliza sababu ya kukata kwake, kisha akajibu, “Nahofia kwamba unapopima, unaweza kuchukua manukato yaliyobaki kwenye vidole vyako na kujipaka mwilini.” Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema baada ya hapo, “Ninahofia kwamba kama utapitisha vidole vyako kwenye mwili wako baada ya kupima manukato, utapata manukato zaidi kuliko Waislamu wengine (na hii hairuhusiwi).

About admin

Check Also

Kupokea Cheti cha Uhuru kutokana na Unafiki na moto wa Jahannam

عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم: من صلى …