Fadhila Za Kusoma Quran Takatifu

Nuru Duniani na Hazina ya Akhera

Abu dharr (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti, “Wakati fulani nilimuuliza Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), ‘Ewe Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), tafadhali naomba unipe nasaha. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema, ‘Shikilia na Taqwa kwa uthabiti, kwa sababu ni kichwa cha matendo yote’ (yaani kitendo kikubwa ilio juu kuliko matendo mengine). Kisha nikasema, ‘Ewe Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), tafadhali nipe nasaha zaidi.” Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: Shikilia sana na usomaji wa Quran Takatifu, hakika hiyo ni nuru kwenu duniani na ni hazina yenu Akhera.”[1]

Njia ya Kusafisha na Kutakasa Moyo

Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Hakika nyoyo hizi zina kutu kama vile chuma unapata kutu wakati maji yanapoigusa.” Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum) wakauliza, “Ewe
Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), ni ipi njia ya kuitakasa?” Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu: “Kukumbuka kifo mara kwa mara na kusoma Qur-aan Takatifu.[2]

Malaika Akilinda Thawabu

Ali (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Mtu anapotumia miswaki kisha akasimama kuswali, Malaika husimama nyuma yake na kusikiliza kwa makini usomaji wake wa Quraan Takatifu. Kisha malaika anamsogelea mpaka aweke kinywa chake juu ya kinywa cha msomaji. Sehemu yoyote ya Qur-aan Takatifu anayoisoma basi inakingwa ndani ya tumbo la Malaika (na baada ya hapo kuhifadhiwa na Allah Ta’ala ). Kwa hivyo, hakikisha kwamba unasafisha kinywa chako kabla ya kusoma Qur-aan Takatifu.[3]


[1] صحيح ابن حبان، الرقم: 361، وقد ذكره المنذري في الترغيب والترهيب، الرقم: 2193، بلفظة “عن”، إشارة إلى كونه صحيحا أو حسنا أو ما قاربهما عنده كما بين أصله في مقدمة كتابه 1/50

[2] شعب الإيمان للبيهقي، الرقم: 1859، وإسناده ضعيف كما في المغني عن حمل الأسفار في الأسفار صــ 323

[3] مسند البزار، الرقم: 550، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 2564: رواه البزار ورجاله ثقات وروى ابن ماجه بعضه إلا أنه موقوف وهذا مرفوع

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …