Umar (radhiyallahu ‘anhu) Akijikumbusha Na Kuhesabiwa Huko Akhera

Licha ya Allah Ta’ala kumbariki Umar (radhiyallahu ‘anhu) kuwa miongoni mwa watu kumi walioahidiwa Jannah hapa duniani, na kuwa khalifa wa pili wa Uislamu, alikuwa mnyenyekevu mno na aliogopa sana kuwajibika mbele ya Allah Ta’ala Siku ya Qiyaamah.

Imeripotiwa kwamba wakati mmoja, Umar (radhiyallahu ‘anhu) aliingia kwenye shamba fulani la matunda huku akiwa amefuatana na Anas (radhiyallahu ‘anhu).

Akiwa kwenye shamba la matunda, alijitenga na Anas (radhiyallahu ‘anhu) na kuenda sehemu tofauti la hilo bustani. Hakujua kwamba Anas (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa akimsikia kwenye sehemu alipokuwa, na akaanza kujisemea mwenyewe na kujikumbusha juu ya kuhesabiwa huko Akhera.

Kisha akajisemea mwenyewe akisema, “Umar bin Khattaab! Watu wanakuita kwa cheo, Ameer-ul-Mu’mineen! kama ukiliona hili kuwa ni jambo zuri, basi naapa kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), Ewe mwana wa Khattaab, kumbuka itakubidi umuogope Allah Ta’ala hapa duniani (kwa kuishi maisha ya taqwa kumcha Allah Ta’ala), ama sivyo atakuadhibu huko Akhera!)” (Muwatta Imaam Maalik #3638)

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …