Imaam Shaafi’ee (rahimahullah) ameandika katika Ikhtilaaful Hadith:
Hatujui hata mmoja wa wake wa Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuondoka majumbani mwao kwenda kuhudhuria Swalaah ya Ijumuah au Swalaah nyingine yoyote msikitini, ingawa wake zake , kwa kuangalia nafasi zao maalum na uhusiano wao na Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), wangekuwa na haki na wastahiki kuliko mwanamake yoyote yule kutimiza faradhi za swalaah msikitini, lakini hawakufanya hivyo.
Kulikua wanawake wengi waliokuwa karibu na Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), kuanzia wanawake wa nyumbani kwake, wake zake waheshimiwa, mabinti zake, watumwa wake wanawake na watumwa wanawake wa watu wa nyumbani kwake, lakini mimi sijui mwanamke mmoja kutoka kwake ambaye aliondoka nyumbani kuhudhuria swalah ya Ijumaah nyuma ya Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), na swalah ya Ijumaah ni wajibu kwa wanaume kwa daraja kubwa kuliko Swalaah zote zingine. Vile vile, hatuna ilm yoyote ya wanawake wakitoka nyumbani kwenda kuhudhuria Swalah ya jamaah, si wakati wa usiku wala mchana, wala hawakuenda hata kwenye msikiti wa Qubaa, ingawa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akienda Qubaa, kuna wakati akipanda mnyama wake na wakati mwingine kwa miguu, wala hawakuenda kwenye misikiti mwengine. Sina shaka kwamba kwa sababu ya uhusiano wao maalum na Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), walikuwa na shauku na matamanio ya kupata wema na malipo, na walijua njia za kupata malipo bora kuliko wanawake wengine, lakini hawakuenda msikitini kwa ajili ya Swalaah.
Sijui hata mmoja katika watangulizi wetu wachamungu kuwaamrisha yoyote katika wanawake wao kuhudhuria Swalaah ya Ijumah wala swalah ya Jamaa, si usiku wala mchana. Lau wangejua kwamba kuna wema wowote kwa wanawake wanaotoka majumbani mwao na kuhudhuria Swalah ya jamaa, bila shaka wangewaelekeza na kuwaruhusu kufanya hivyo. Bali imepokewa kutoka kwa Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema: “Swala ya mwanamke ndani kabisa ya chumba chake cha kulala ni bora kuliko Swalah yake ndani ya chumba cha jumuia ya nyumbani kwake, na Swalaah yake ndani ya chumba cha jumuia ni bora kuliko Swalaah yake msikitini.”[1]
[1] ولم نعلم من أمهات المؤمنين امرأة خرجت إلى جمعة ولا جماعة في مسجد وأزواج رسول الله صلى الله عليه وسلم بمكانهن من رسول الله صلى الله عليه وسلم أولى بأداء الفرائض … وقد كان مع رسول الله صلى الله عليه وسلم نساء من أهل بيته وبناته وأزواجه ومولياته وخدمه وخدم أهل بيته فما علمت منهن امرأة خرجت إلى شهود جمعة والجمعة واجبة على الرجال بأكثر من وجوب الجماعة في الصلوات غيرها ولا إلى جماعة غيرها في ليل أو نهار ولا إلى مسجد قباء فقد كان النبي صلى الله عليه وسلم يأتيه راكبا وماشيا ولا إلى غيره من المساجد وما أشك أنهن كن على الخير بمكانهن من رسول الله صلى الله عليه وسلم أحرص وبه أعلم من غيرهن … وما علمت أحدا من سلف المسلمين أمر أحدا من نسائه بإتيان جمعة ولا جماعة من ليل ولا نهار ولو كان لهن في ذلك فضل أمروهن به وأذنوا لهن إليه بل قد روي والله أعلم عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال صلاة المرأة في بيتها خير من صلاتها في حجرتها وصلاتها في حجرتها خير من صلاتها في المسجد أو المساجد (اختلاف الحديث صـ 625-626)