Qunoot

1. Ni Sunnah kusoma Qunoot katika rakaa ya pili ya Alfajiri. Qunoot itasomwa katika rakaa ya pili pindi unaposimama baada ya rukuu. Mtu atasoma kwanza tahmiid (ربنا لك الحمد) na baada ya hapo ataisoma Qunout.

2. Wakati wa kusoma Qunoot, mtu atainua mikono yake sambamba na kifua chake na kufanya dua kwa namna jinsi anainuaga mikono yake kifuani na kuomba dua baada ya Swalaah. Lakini, usipitishe mikono yako usoni baada ya Qunuut. Qunuut ya Swalah ya Alfajiri ni:

اَللّٰهُمَّ اهْدِنِيْ فِيْمَنْ هَدَيْتَ وَعَافِنِيْ فِيْمَنْ عَافَيْتَ وَتَوَلَّنِيْ فِيْمَنْ تَوَلَّيْتَ وَبَارِكْ لِيْ فِيْمَا أَعْطَيْتَ وَقِنِيْ شَرَّ مَا قَضَيْتَ إِنَّكَ تَقْضِيْ وَلَا يُقْضٰى عَلَيْكَ إِنَّهُ لَا يَذِّلُّ مَنْ وَّالَيْتَ وَلَا يَعِزُّ مَنْ عَادَيْتَ تَبَارَكْتَ رَبَّنَا وَتَعَالَيْتَ فَلَكَ الْحَمْدُ عَلٰى مَا قَضَيْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوْبُ إِلَيْكَ وَصَلّٰى اللهُ عَلٰى النَّبِيِّ وآلِهِ

Ewe Mwenyezi Mungu , niongoze pamoja na wale uliowaongoza. Nijaalie wepesi pamoja na wale uliowajaalia wepesi, na nisimamie mambo yangu (na unisaidie) pamoja na wale uliowasimamia (na ukawasaidia), nijazie baraka ndani ya vitu ulivyonipa, niokoe na ubaya ya yale uliyoyahukumu. Hakika Wewe ni Mwenye kuhukumu (mambo yote) na hakuna mwenye kufanya mamuzi dhidi Yako. Yeyote aliye chini ya ulinzi wako, hawezi kufedheheshwa, na wale uliowafanya kuwa adui zako hawatapata heshima kamwe. Mola wetu, Wewe ni mwingi wa baraka na Mkubwa Zaidi. Sifa njema zote ni zako peke yako kwa maamuzi unayofanya. Ninakuomba msamaha na naelekea Kwako kwa toba na baraka za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) zimshukie Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) na familia yake.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

3. Soma Dua ya Tashahhud. اَلتَّحِيَّاتُ الْمُبَارَكَاتُ الصَّلَوَاتُ الطَّيِّبَاتُ لِلّٰهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ …