Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 2

4. Soma Surah Yaseen kila asubuhi na jioni.

Ibnu Abbaas (radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba, “Yoyote anayesoma Sura Yaaseen asubuhi, kazi yake ya siku hiyo nzima itarahisishwa, na yoyote atakayeisoma mwisho wa siku, kazi yake mpaka asubuhi itarahisishwa.”[1]

Jundub (radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Sura Yaseen usiku kwa nia ya kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), atasamehewa madhambi yake (madogo).”[2] (Katika riwaya ya Shu’abul Imaan, imetajwa kwamba mwenye kusoma Sura Yaaseen, atasamehewa madhambi yake madogo. Hadithi hii haielezi wazi kuisoma usiku. Hivyo basi, fadhila ya madhambi ya mtu kusamehewa kupitia kisomo chake itapatwa kwa kuisoma wakati wowote wa usiku au mchana.)[3]

5. Soma Surah Mulk (Tabaarak) kabla ya kulala.

Imepokewa kwamba Abdullah bin Mas’ud (radhiyallahu ‘anhu) amesema, “Mwenye kusoma Sura Mulk kila usiku, basi kwa ajili ya surah hii, Allah Ta’ala Atamlinda na adhabu ya kaburi. Wakati wa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) sisi (Maswahabah radhiyallahu anhum) tulikuwa tukiita surah hii kwa jina la ‘Al Maani’ah (Mwenye kumkinga mtu na adhabu ya kaburi)’. Ni sura ambayo mwenye kuisoma kila usiku bila shaka amefaulu mengi na amefanya mema.”[4]

Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Hakika mimi natamani (Surah Mulk) iwe katika moyo wa kila mtu katika Ummah wangu.”[5]

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ametaja, “Hakika kuna surah kubwa ndani ya Quraan Majeed ambayo ina aya thalathini. Itamuombea mtu (anayeisoma kwa muda) mpaka apate msamaha. Sura hii ni Sura Tabaarak.”[6]


[1] سنن الدارمي، الرقم: 3462، وفي سنده ضعف

[2] صحيح ابن حبان، الرقم: 2574

[3] شعب الإيمان، الرقم:2235، وقال الصنعاني في التنوير 10/353: رمز المصنف لضعفه

[4] عمل اليوم والليلة للنسائي، الرقم: 711، وقال العلامة المنذري رحمه الله في الترغيب والترهيب، الرقم: 2453: رواه النسائي واللفظ له والحاكم وقال: صحيح الإسناد

[5] المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 11616، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 11429: رواه الطبراني وفيه إبراهيم بن الحكم بن أبان وهو ضعيف

[6] سنن الترمذي، الرقم: 2891، وقال: هذا حديث حسن

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …