Hofu Ya Uthman (radhiyallahu ‘anhu) kwa ajili ya Akhera

Haani (rahimahullah), mtumwa aliyeachwa huru wa ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu), anataja kwamba wakati ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) anaposimama kaburini, alikuwa akilia sana hadi ndevu zake zikilowa kwa machozi yake.

Mtu mmoja akamuuliza, “Tunaona kwamba unapokumbuka Jannah na Jahannam na kuzijadili, hauathiriki hadi unaanza kulia, lakini unaposimama kaburini tunakuona unaingiwa na hofu hadi unaanza kulia sana. Hili ni kwa sababu gani?”

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu, “Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, Kaburi ni hatua ya kwanza kutoka hatua za Akhera. Kama mtu akifaulu hatua hii na kupata wokovu, basi kuna matumaini kwamba hatua zinazokuja zitakuwa rahisi zaidi, na ikiwa mtu hatofaulu hatua hii na kupata wokovu, basi hatua zinazokuja zitakuwa ngumu zaidi na kali zaidi kwake.” (Sunan Tirmizi #2308)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …