Qunoot

3. Ni sunna kuswali Witr kila siku katika kipindi chote cha mwaka. Swala ya Witr itatekelezwa baada ya kuswali Fardh na Sunnah za Swalah ya Esha. Kwa mwaka mzima, mtu anaposwali Witr, hatosoma Qunoot. Lakini, ni sunna kusoma Qunout kwenye Witr katika kipindi cha pili ya Ramadhaan (tangu 15 Ramadhani hadi mwisho wa Ramadhani). Qunoot ya Witr ni:

اَللّٰهُمَّ إِنَّا نَسْتَعِيْنُكَ وَنَسْتَغْفِرُكَ وَنَسْتَهْدِيْكَ وَنُؤْمِنُ بِكَ وَنَتَوَكَّلُ عَلَيْكَ وَنُثْنِيْ عَلَيْكَ الْخَيْرَ كُلَّهُ نَشْكُرُكَ وَلَا نَكْفُرُكَ وَنَخْلَعُ وَنَتْرُكُ مَنْ يَّفْجُرُكَ اَللّٰهُمَّ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَلَكَ نُصَلِّيْ وَنَسْجُدُ وَإِلَيْك نَسْعٰى وَنَحْفِدُ نَرْجُوْ رَحْمَتَكَ وَنَخْشٰى عَذَابَكَ إِنَّ عَذَابَكَ الْجِدَّ بِالْكُفَّارِ مُلْحِقٌ

اَللّٰهُمَّ اهْدِنِيْ فِيْمَنْ هَدَيْتَ وَعَافِنِيْ فِيْمَنْ عَافَيْتَ وَتَوَلَّنِيْ فِيْمَنْ تَوَلَّيْتَ وَبَارِكْ لِيْ فِيْمَا أَعْطَيْتَ وَقِنِيْ شَرَّ مَا قَضَيْتَ إِنَّكَ تَقْضِيْ وَلَا يُقْضٰى عَلَيْكَ إِنَّهُ لَا يَذِّلُّ مَنْ وَّالَيْتَ وَلَا يَعِزُّ مَنْ عَادَيْتَ تَبَارَكْتَ رَبَّنَا وَتَعَالَيْتَ فَلَكَ الْحَمْدُ عَلٰى مَا قَضَيْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوْبُ إِلَيْكَ وَصَلّٰى اللهُ عَلٰى النَّبِيِّ وآلِهِ

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Tunaomba msaada wako na tunaomba msamaha kutoka kwako na sisi tunatafuta mwongozo Wako. Tunakuamini, tunaweka tumaini wetu Kwako. Tunakusifu kwa kila aina ya fadhila (juu yetu). Tunatoa shukrani zetu Kwako na sisi sio watu wa kukufuru. Tunajitenga na kumwacha yule anayekuasi. Ewe Allah Ta’ala! Wewe tu tunakuabudu na kwa ajili Yako tunaswali na tunasujudu. Tunakimbilia Kwako na kwa haraka. Tunataraji rehma zako na tunaiogopa adhabu Yako kali. Hakika adhabu yako kali itawafikia makafiri.

Ewe Mwenyezi Mungu , niongoze pamoja na wale uliowaongoza. Nijaalie wepesi pamoja na wale uliowajaalia wepesi, na nisimamie mambo yangu (na unisaidie) pamoja na wale uliowasimamia (na ukawasaidia), nijazie baraka ndani ya vitu ulivyonipa, niokoe na ubaya ya yale uliyoyahukumu. Hakika Wewe ni Mwenye kuhukumu (mambo yote) na hakuna mwenye kufanya mamuzi dhidi Yako. Yeyote aliye chini ya ulinzi wako, hawezi kufedheheshwa, na wale uliowafanya kuwa adui zako hawatapata heshima kamwe. Mola wetu, Wewe ni mwingi wa baraka na Mkubwa Zaidi. Sifa njema zote ni zako peke yako kwa maamuzi unayofanya. Ninakuomba msamaha na naelekea Kwako kwa toba na baraka za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) zimshukie Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) na familia yake.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

3. Soma Dua ya Tashahhud. اَلتَّحِيَّاتُ الْمُبَارَكَاتُ الصَّلَوَاتُ الطَّيِّبَاتُ لِلّٰهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ …