Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo fanya dua.

Swalawaat Ibrahimiyyah ni ifuatavyo:

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَّعَلٰى اٰلِ مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى اٰلِ إِبْرَاهِيْمَ  وَبَارِكْ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَّعَلٰى اٰلِ مُحَمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى اٰلِ إِبْرَاهِيْمَ فِيْ الْعَالَمِيْنَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَّجِيْدٌ

Ewe Allah Ta’ala! Mteremshie rahma zako maalum kwa Sayyidina Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na pia familia ya Sayyidina muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam) kama ulivyoteremsha rehma zako maalum kwa Sayyidina Ebrahim (‘alaihi salaam) na familia ya Sayyidina Ebrahim (‘alaihi salaam) na mteremshie baraka zako maalum Sayyidina Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na pia familia ya Sayyidina muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam) kama ulivyoteremsha baraka zako maalum kwa Sayyidina Ebrahim (‘alaihi salaam) na familia ya Sayyidina Ebrahim (‘alaihi salaam) katika walimwengu wote (yaani miongoni mwa watu wa vipindi vyote). Hakika Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mkubwa.

Katika qa’dah ya mwisho, mtu anaweza kusoma dua ifuatayo ambayo imepokewa katika Hadith:

اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ ظَلَمْتُ نَفْسِيْ ظُلْمًا كَثِيرًا وَلَا يَغْفِرُ الذُّنُوْبَ إِلاَّ أَنْتَ فَاغْفِرْ لِيْ مَغْفِرَةً مِّنْ عِنْدِكَ وَارْحَمْنِيْ إِنَّكَ أَنْتَ الْغَفُوْرُ الرَّحِيْم

Ewe Allah Ta’ala! Nimejidhulumu kupita kiasi (kwa kufanya madhambi), na Wewe ndiye pekee mwenye uwezo kusamehe madhambi, basi nisamehe kwa msamaha maalum kutoka upande Wako na unirehemu, kwani Wewe peke ndiye Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.

8. Baada ya kumaliza dua yako, toa salamu kwa kusema,

اَلسَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهْ

huku ukigeuza kichwa chako upande wa kulia, na kisha tena ukigeuza kichwa chako upande wa kushoto.

9. Usiinamishe au kutikisa kichwa wakati wa kutoa salaam.

10. Geuza uso wako pande zote mbili kwa kiasi ambacho mtu aliye nyuma ataweza kuona shavu lako.

11. Baada ya salamu, soma mara tatu استغفر الله.

12. Shiriki katika dua kwa sababu huu ni wakati wa kukubaliwa dua.

13. Soma Tasbih Faatimi baada ya kila Swalaah. Tasbeeh Faatimi ni mtu kusoma mara 33 Subhaanallah, 33 Alhamdulillah, 33 Allahu Akbar, na kukamilisha mia kwa kusoma:

لَا إِلٰهَ إلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْر

Amna apasae kuabudia isipokuwa Allah Ta’ala peke yake, ambaye hana mshirika. Ufalme ni wake (wa ulimwengu wote), na sifa njema zote ni Zake tu, na Yeye pekee ndiye Muweza wa kila kitu.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

3. Soma Dua ya Tashahhud. اَلتَّحِيَّاتُ الْمُبَارَكَاتُ الصَّلَوَاتُ الطَّيِّبَاتُ لِلّٰهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ …