Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 1

Kuna baadhi ya surah ambazo zinatakiwa kusomwa kwenye nyakati maalum wakati wa usiku na mchana au katika siku fulani ndani ya week. Ni mustahab kwa mtu kusoma surah hizi kwa muda wake.

1. Soma Surah Kaafirun kabla ya kulala

Imepokewa kutoka kwa Jabalah bin Haarithah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Unapolala, basi soma Sura Kafirun mpaka mwisho wa surah, kwani kwa hakika kuisoma surah hii ni njia ya kujiepusha na shirki.”[1]

2. Soma Surah Ikhlaas, Surah Falaq na Surah Naas mara tatu kila asubuhi na jioni.

Abdullah bin Khubaib (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia: Wakati mmoja, wakati wa usiku na mvua, tulitoka kwenda kumtafuta Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ili atuongoze katika Swalaah. Kisha nikakutana na Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia: “Soma.” Lakini (bila kujua nini cha kusoma,) sikusoma chochote. Aliniambia kwa mara ya pili, “Soma.” Lakini (bila kujua nini cha kusoma,) sikusoma chochote. Aliniambia kwa mara ya tatu, “Soma.” Kisha nikauliza, “Nisome nini ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)? Mtume (sallallahu’alaihi wasallam) akajibu, “Soma Sura Ikhlaas na Mu’awwadhatain (yaani Surah Falaq na Surah Naas) asubuhi na jioni mara tatu, itakutosheleza kuwa kinga ya madhara yote.”[2]

3. Soma Surah Waaqi’ah usiku.

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Mwenye kusoma Sura Waaqi’ah kila usiku, ufukara na umasikini hautampata kamwe.” Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) anasema: “Nimewaagiza mabinti zangu waisome surah hii kila usiku.”[3]

Pindi Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) alipolala kwenye kitanda chake cha mauti na dakika zake za mwisho ulikuwa unakaribia, Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu), ambaye alikuwa Khalifah wakati huo, alikuja kumtembelea. Wakati wa ziara hiyo, Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alimuuliza, “Je, niagize upewe posho?” Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Sina haja nayo.” Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Posho itakuwa ya mabinti zako (baada ya kufariki kwako).” Kwa hili, Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Je, unakhofu kwamba mabinti zangu watakuwa maskini? (Usiwe na khofu hii kwa sababu) Nimewaelekeza mabinti zangu wasome Surah Waaqi’ah kila usiku. Hakika mimi nilimsikia Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema, ‘Mwenye kusoma Sura Waaqi’ah kila usiku, ufukara hautampata.[4]


[1] المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 2195، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17033: رواه الطبراني ورجاله وثقوا

[2] سنن الترمذي، الرقم: 3575، وقال: هذا حديث حسن صحيح غريب من هذا الوجه

[3] عمل اليوم والليلة لإبن السني، الرقم: 680 ، شعب الإيمان للبيهقي، الرقم: 2269، وقال المباركفوري في مرعاة المفاتيح 7/255:  وحديث ابن مسعود أخرجه أيضاً ابن السني ونسبه السيوطي في الإتقان للبيهقي والحارث ابن أبي أسامة وأبي عبيد وإسناد ابن السني حسن

[5] أسد الغابة: 3/77

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …