Qa’dah Na Salaam

3. Soma Dua ya Tashahhud.

اَلتَّحِيَّاتُ الْمُبَارَكَاتُ الصَّلَوَاتُ الطَّيِّبَاتُ لِلّٰهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللّٰهِ وَبَرَكَاتُهُ سَلَامٌ عَلَيْنَا وَعَلٰى عِبَادِ اللّٰهِ الصَّالِحِيْنَ أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَّسُولُ اللّٰهِ

Ibaadah zote za Kisomo zilizobarikiwa, ibaadah za kimwili ni za Allah Ta’ala. Amani ya Allah Ta’ala iwe juu yako, ewe Nabi (Sallallahu ‘alaihi wasallam), na rehma na baraka za Mwenyezi Mungu (ziwe juu yako). Amani zishuke juu yetu na juu ya waja wote wema wa Allah Ta’ala. Nashuhudia ya kwamba hakuna apasae kuabudiwa isipokuwa Allah Ta’ala, na nashuhudia kwamba Sayyidina Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ni Mtume wa Allah Ta’ala.

4. Utakaposema إِلَّا الله inua kidole cha shahada kuelekea kibla na uiache katika hali hio mpaka mwisho wa qa’dah. Wakati wa kuinua kidole cha shahada, weka macho yako kwenye kidole cha shahada mpaka mwisho wa Swalaah.

5. Ikiwa unaswali rakaa tatu au nne kisha baada ya kusoma dua ya tashahhud katika qa’da ya kwanza, basi soma pia swalah alan Nabi. Wakati wa kusoma swalah alan Nabi, soma mpaka jina lililobarikiwa la Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam). Baada ya hapo simama kwa ajili ya rakaa ya tatu. Usiombe dua baada ya swalah alan Nabi.

6. Wakati unasimama kwa ajili ya rakaa ya tatu, chukua usaidizi kutoka ardhini kwa kuweka mikono yako miwili juu yake. Vile vile utachukua usaidizi wa mikono utakaposimama kwenye rakaa ya nne.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo …