binary comment

Sunnah na Adabu Za Kusoma Qur’an Takatifu 8

23. Ikiwa umehifadhi sehemu yoyote ya Qur’an Majeed basi hakikisha kwamba unapitia na kufanya muraaja’a mara kwa mara ili usiisahau. Hadith imetahadharisha juu ya kupuzia kisomo cha Quraan Majeed na kusahau ulichohifadhi.

Abu Muusa Ash’ari (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam ) alisema, “Ichunge (na ilinde) Quraan Takatifu. Naapa kwa Ambaye uhai wangu umo mikononi Mwake, inaweza (Qur’an Majeed) kutoroka haraka kutoka moyoni kuliko ngamia anavyoweza kutoroka kutoka kwenye kamba yake (ambayo amefungwa).”

Anas bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Thawabu ya matendo mema ya Ummah wangu zililetwa mbele yangu, hadi kadiri (nilionyeshwa ujira) wa mtu kuokota kipande kidogo cha uchafu kilichokuwa chini msikitini, na dhambi za Ummah wangu zililetwa mbele yangu, na sikuona dhambi kubwa kuliko dhambi ya mtu aliyesahau sura au aya ya Quran Takatifu aliyobarikiwa nacho”

Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Mfano wa mwenye kuhifadhi Qur’an Majeed ni kama mtu aliyefunga ngamia. Akiendelea kuwachunga atawaweka na usalama, na akiwaacha bila kuwafunga watamwacha.”

Imepokewa kutoka kwa Sa’d bin Ubaadah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Hakuna mtu anayejifunza Qur’an Takatifu kisha akaisahau, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)
Siku ya Qiyaamah kama mwenye ukoma.”

Maelezo:

1. Katika Hadith hii, dhambi ya kusahau ayah au surah ya Quran Takatifu inaelezwa kuwa ni dhambi mbaya zaidi. Sababu yake ni kwamba aonyesha shukrani kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kwa hii neema kubwa ya Qur’an Majeed kwa kughafilika na kisomo chake na hivyo kusahau yale ambayo mtu amebarikiwa nayo.

2. Baadhi ya Maulamaa wameeleza kuwa maonyo yaliyoelezwa katika Hadith hii ni kwa mwenye kupuuza kusoma Quraan Majeed na kusahau yale aliyoyaweka kwenye kumbukumbu. Maulamaa wengine wanaona kwamba maonyo haya ni kwa ajili ya yule ambaye anapuuza usomaji wa Qur’an Majeed kwa kiasi kwamba yeye sio tu kusahau kile alichoweka kwenye kumbukumbu, lakini pia husahau jinsi ya kusoma Quran Majeed.

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …