Bashara Za Jannah

Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia yafuatayo:

Wakati fulani nilikuwa na Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) katika bustani mmoja wa Madina Munawwarah alipokuja mtu na kuomba ruhusa ya kuingia kwenye bustani hiyo. Aliposikia ombi la mtu huyo, Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia: “Mruhusu aingie na umpe bashara ya daraja la juu katika Jannah.” Hivyo nikamfungulia mlango mtu huyo na nikamkuta si mwingine bali ni Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu). Nilimfikishia bashara alizozitaja Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na akamtukuza Allah Ta’ala kwa shukurani.

Muda mfupi baadaye, mtu mwingine alikuja na kuomba kuingia kwenye bustani hiyo. Kusikia ombi lake,
Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia: “Mruhusu aingie na umpe bashara ya daraja la juu katika Jannah. ” Hivyo nikamfungulia mlango mtu huyo, na nikakuta kwamba hakuwa mwingine bali ni ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu). Nilimfikishia bashara alizozitaja Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na akamhimidi Allah Ta’ala kwa shukurani.

Baada ya muda fulani, mtu mwingine aliomba ruhusa ya kuingia kwenye bustani hiyo. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia: “Mruhusu aingie, na umpe bashara ya daraja la juu katika Jannah, pamoja na mtihani atakayokutana nayo.” Nilipofungua mlango, nilikuta mtu huyo si mwingine bali ni ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu). Nilimjulisha yale aliyoyataja Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ambapo akamtukuza Allah Ta’ala kwa kushukuru kisha akasema: “Kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) pekee tunaomba msaada.” (Sahih Bukhari #3693)

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …