Rakaa ya Pili

1. Unapoinuka kutoka kwenye sajdah, kwanza inua paji la uso na pua; kisha viganja vya mkoni na mwisho magoti.

2. Ukiwa unasimama kwa ajili ya rakaa ya pili, chukua usaidizi kutoka ardhini kwa kuweka mikono yako miwili juu yake.

3. Tekeleza rakaa ya pili kama kawaida (bila ya kusoma Dua- ul- Istiftaah)

Qa’dah Na Salaam

1. Baada ya sajda ya pili ya rakaa ya pili, kaa katika mkao wa tawarruk, yaani, kaa kwenye kitako cha kushoto na utoe mguu wa kushoto kutoka chini ya muundi wa mguu wa kulia. Weka mguu wa kulia ukiwa umesimama na vidole vya miguu vikielekea kibla.

Maelezo: Kukaa katika mkao wa tawarruk kutafanyika katika swala ambayo ina qa’dah moja yaani rakaa mbili na qa’da ya mwisho ya rakaa nne. Ama qa’dah ya kwanza ya rakaa tatu au nne, mtu atakaa katika mkao wa iftiraash yaani ataweka mguu wa kulia pamoja na vidole vya miguu vikielekea kibla na mtu atakaa juu ya mguu wa kushoto akiuweka sawa chini.

2. Wakati wa kukaa kwenye tashahhud, funga vidole vitatu vya mkono wa kulia yaani kidole cha kati na vidole viwili kando yake. Kidole cha shahaadah na kidole gumba vitaachwa wazi lakini kidole gumba kitaunganishwa kando na kidole cha shahaadah. Kuhusu mkono wa kushoto, acha vidole vimetandazwa kwenye ukingo wa paja. Vidole vitaachwa katika hali yake asili na haitaunganishwa pamoja.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo …