Muislamu Wa Kwanza Kufanya Hijrah Pamoja Na Familia Yake

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameondoka kwenda Abyssinia, akihijiria pamoja na mke wake mheshimiwa, Ruqayyah (radhiyallahu ‘anha), binti Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Habari za hali yao zilicheleweshwa, na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akawa na wasiwasi na alikuwa akitaka kutoka Makkah Mukarramah kupata habari zao. Hatimaye, mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) na kumpa taarifa kuwahusu.

Katika tukio hili, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “ Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ni mtu wa kwanza kufanya Hijrah katika njia ya Allah Ta’ala na familia yake baada ya Nabii Lut (‘alaihi salaam).

Katika riwaya nyingine, imetajwa kwamba wakati Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alivyokusudia kufanya Hijrah huko Abyssinia, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimwambia, “Mchukuwe Ruqayyah (radhiyallahu ‘anha) nawe. Ninahisi kwamba kila mmoja wenu atamuunga mkono na kumtia moyo mwenzake kuvumilia.”

Baada ya muda kutoka wakati wa kuondoka kwao, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimwomba Asmaa (radhiyallahu ‘anha), binti wa Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu), kuwaulizia hali yao. Baada ya kuuliza, alimkuta Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) pamoja na baba yake mheshimiwa, Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu).

Akasema: “Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Nilipata habari kwamba Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kwa sasa anasafiri kuelekea baharini katika hali ya kwamba mke wake, Ruqayyah (radhiyallahu ‘anhu) amekaa juu ya punda.”

Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akafurahi na akasema, “Ewe Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu)! Hao ndio watu wa kwanza duniani kufanya Hijrah katika njia ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) baada ya Manabii wawili, Nabi Lut (‘alaihis salaam) na Nabi Ebrahim (‘alaihis salaam), kuhijiria.”

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …