Sunnah na Adabu Za Kusoma Qur’an Takatifu 7

22. Baada ya kumaliza kusoma Quraan Majeed yote basi soma dua ifuatayo:

اَللّٰهُمَّ ارْحَمْنِيْ بِالْقُرْآنْ وَاجْعَلْهُ لِيْ إِمَاماً وَّهُدًى وَّرَحْمَةً اَللّٰهُمَّ ذَكِّرْنِيْ مِنْهُ مَا نَسِيْتُ وَعَلِّمْنِيْ مِنْهُ مَا جَهِلْتُ وَارْزُقْنِيْ تِلَاوَتَهُ آنَاءَ اللَّيْلِ وَأَطْرَافَ النَّهَارِ وَاجْعَلْهُ لِيْ حُجَّةً يَا رَبَّ الْعَالَمِيْنَ

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Nimiminie rehema Yako makhsusi kupitia Quran Takatifu, na unijaalie iwe imamu kwangu (njia ya kuniongoa katika maisha yangu), njia ya mwongozo na njia ya rehema. Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Nisaidie kukumbuka sehemu hiyo ya Quraan Majeed nisiusahahu, na nifundishe sehemu hiyo ya Quraan Majeed nisiyoijua, na nibariki niisome Quraan Majeed usiku na mchana, na uijaalie kuwa ni dalili na hoja kwangu (Siku ya Qiyaamah), Ewe Mola wa ulimwengu!

23. Ikiwa umehifadhi sehemu yoyote ya Qur’an Majeed basi hakikisha kwamba unapitia na kufanya muraaja’a mara kwa mara ili usiisahau. Hadith imetahadharisha juu ya kupuzia kisomo cha Quraan Majeed na kusahau ulichohifadhi.

Abu Muusa Ash’ari (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam ) alisema, “Ichunge (na ilinde) Quraan Takatifu. Naapa kwa Ambaye uhai wangu umo mikononi Mwake, inaweza (Qur’an Majeed) kutoroka haraka kutoka moyoni kuliko ngamia anavyoweza kutoroka kutoka kwenye kamba yake (ambayo amefungwa).”

About admin

Check Also

Dua Baada Ya Kula 1

Dua ya kwanza: Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alitupa chakula na vinywaji na kutufanya Waislamu.

Dua ya pili Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alinipa chakula hiki kula, na alinipa bila juhudi yoyote au jitihada kutoka upande wangu.

Maelezo: Mu'aadh bin Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, "Yoyote anayekula chakula chochote na baada ya hapo anasoma Dua iliyotajwa hapo juu, dhambi zake zilizopita na za baadaye (ndogo) zitasamehewa. "