1. Soma takbira na ukae katika hali ya jalsah.
2. Weka mguu wa kulia katika hali ukiwa umesimama huku vidole vyake vya miguu vikikandamizwa chini na vielekee kibla. Weka mguu wa kushoto pande na uukalie.
3. Kaa kwa namna ambayo mapaja yako yote yameunganishwa pamoja.
4. Weka mikono juu ya mapaja na vidole viwe pamoja na pia yawekwe kwenye sehemu ambapo goti linaanzia.
5. Macho yawe yanaangalia kwenye sehemu ya kusujudu ukiwa kwenye jalsah.
6. Baki katika hali ya jalsah huku mwili ukiwa umetulia kabla ya kuendelea kwenye sajda ya pili.
7. Soma dua ifuatayo katika jalsah:
اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِيْ، وَارْحَمْنِيْ، وَعَافِنِيْ، وَاجْبُرْنِيْ، وارْفَعْنِيْ، وَاهْدِنِيْ، وَارْزُقْنِيْ
Ewe Allah Ta’ala Nisamehe, Nirehemu, Niweke katika hali ya utulivu, Niondolee udhaifu wangu, Nipandishe daraja, Niongoze na unibariki kwa riziki.
8. Soma takbira na uende kwenye sajdah ya pili kama kawaida.
9. Inuka kutoka kwenye sajdah ya pili hadi kwenye nafasi ya kukaa kwa muda mfupi. Mkao huu unaitwa Jalsatul Istiraahah. Ni sunna kuanza takbira wakati wa kuinuka kutoka kwenye sajdah na kuimaliza takbira baada ya kufikia nafasi ya qiyaam.