Kununua Kisima katika Jannah

Maswahaabah (radhiya llaahu ‘anhum) walipohamia Madinah Munawwarah, maji Yaliopatikana Madinah Munawwarah yalikuwa vigumu kwao kunywa kutokana na maji kuwa chungu. Hata hivyo, kulikuwa na Myahudi mmoja anayeishi Madinah Munawaarah ambaye alikuwa na kisima chenye maji matamu kilichoitwa Roomah. Alikuwa akiuza maji ya kisima chake kwa Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum).

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwauliza Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum), “Ni nani atakayenunua kisima cha Roomah kutoka kwa huyu Myahudi na kukitoa kwa manufaa ya Waislamu ili awe sawa na Waislamu katika kuteka maji yake? na atapata kisima katika Jannah badala ya kisima hiki?”

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alikwenda kwa Myahudi ambaye alikuwa mmiliki wa kisima na akajitolea kununua Roomah kutoka kwake. Lakini, Myahudi huyo alikataa kukiuza kile kisima kizima, na badala yake aliuza nusu tu ya kisima hicho kwa ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) kwa dirham elfu kumi na mbili.

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alitoa mara moja kwa manufaa ya Waislamu. Baada ya hapo, Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) akamwambia Myahudi: “Ukitaka tunaweza kutundika ndoo mbili juu ya kisima (ili tuweze kutumia kisima hicho kwa wakati mmoja), au ukipenda naweza kutumia kwa siku moja na wewe unaweza kuitumia siku inayofuata.” Myahudi akajibu kwamba alipendelea kubadilishana siku moja moja na ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) kwa ajili ya matumizi yake vizuri.

Baada ya hapo, ilipofika siku ya ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu), Waislamu walikuwa wakija kisimani na kuteka maji ya kutosha ya kudumu kwa muda wa siku mbili. Kuona kuwa Waislamu hawanunui tena maji kutoka kwake, Myahudi akamwambia ‘Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu), “Umeharibu kisima changu (kwani siwezi tena kuuza maji kwa watu)! Kwa nini usinunue nusu nyingine kutoka kwangu.” ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alinunua nusu nyingine ya kisima kutoka kwake kwa dirham elfu nane na pia akaitoa kwa manufaa ya Waislamu. (Istee‘aab juzuu ya 3 # 157)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …