Sajdah

1. Soma takbira na kisha nenda kwenye sajdah.

2. Weka mikono kwenye magoti huku ukiendelea kwenda kwenye sajdah.

3. Kwanza weka magoti chini, kisha mikono, na mwisho paji la uso na pua kwa pamoja.

4. Vidole viwekwe kwa pamoja na vielekee kibla.

5. Weka mikono yako chini kwa njia ambayo vidole na masikio yapo kwenye mstari sawa sawa na sehemu za chini za viganja (Yaani vifundo vya mikono) vinaendana na mabega.

6. Weka viungo vya mwili karibu pamoja na vibane kwa nguvu bila kuruhusu nafasi yoyote kati kati.

7. Hakikisha tumbo limeunganishwa na mapaja yote mawili na mikono yawe pempeni.

8. Weka miguu yote miwili chini na vidole vya miguu vikitazama kibla. Acha nafasi sawa sawa na mkono mmoja kati ya miguu yako katika sajdah.

9. Macho yawe yanaangalia sehemu ya sajdah.

10. Soma tasbeeh ifuatayo mara tatu au idadi yoyote isiyo yakugawanyika:

سُبْحَانَ رَبِّيَ الْأَعْلٰى

Utukufu ni wa Mola Wangu aliye mkubwa.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo …