Asubuhi wakati Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipochomwa kisu, kijana mmoja alimtembelea na kumwambia, “Ewe Ameer-ul-Momineen! Furahi kwa bashara kutoka kwa Allah Ta’ala! Wewe ni miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na wewe ni miongoni mwa waliosilimu siku za mwanzo kabisa. Baada ya hapo ukachaguliwa kuwa khalifa na ukafanya uadilifu katika utawala wako wote, na hivi karibuni utakufa shahidi!”
Aliposikia haya, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema, “Natamani vipengele vyote hivi (ulivyovitaja) vinisaidie ili pasiwe na kitu chochote kunipinga (siku ya qiyamah), na pasiwe na chochote kunipendelea (yaani Ningefurahi ikiwa matendo yangu yote mema yanatosha tu kukabiliana na udhaifu wangu na nibaki bila chochote kwa niaba yangu na hakuna chochote chenye kitakuwa kinyume kwangu)”.
Wakati kijana huyu alipogeuka kuondoka, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliona kwamba vazi lake la chini lilikuwa limepitiriza vifundo vya miguu na linagusa chini. Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliamrisha arudishwe, na kisha akamwambia, “Ewe mpwa wangu! Inua nguo yako ya chini (na ivae juu ya vifundo vya miguu yako kwa mujibu wa sunna), kwa sababu hii ni safi zaidi kwa ngui yako na ni njia ya kumcha Allah Ta‘ala” (Bukhaari #3700).