Kuwa Mlaini na Mpole Unapojishughulisha na Watu:

‘Ataa bin Farrookh (rahimahullah) anasimulia yafuatayo:

Wakati mmoja, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alinunua kiwanja kutoka kwa mtu fulani. Baada ya kununua ardhi, ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimsubiri mtu huyo aje kuchukua pesa zake. Lakini mtu huyo hakuja.

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alipokutana na mtu huyo baadaye, alimuuliza, “Kwa nini hukuja kuchukua pesa zako?” Yule mtu akajibu, “Sababu ya mimi kutokuja kuchukua pesa ni kwamba nilihisi kuwa hukunilipa bei nzuri ya shamba! Kila mtu niliyekutana naye alinisuta kwa kukuuzia shamba kwa bei hii.” ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza, “Hii ndiyo sababu ya wewe kutokuja kuchukua pesa zako?” Yule mtu akajibu kwa kusema ndio.

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) akamwambia, “Ninakupa hiyari ya kufuta mkataba wetu na kuchukua ardhi yako au kuacha mauzo kama yalivyo na kuchukua pesa zako.”

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) baada ya hapo akamueleza sababu ya kumpa chaguo la kukata mauzo au kuiruhusu iendelee kusema, “Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa ameomba du‘a kwa mtu ambaye ni mpole wakati wa kufanya biashara. Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, ‘Allah Ta’ala ambariki mtu huyo na Jannah ambaye anakuwa mlaini na mpole wakati anaponunua, kuuza, kufanya malipo au kuomba malipo. (Musnad Ahmed #410)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …