8. Kwa kukaribia ramadhaani na pia ndani ya ramadhaani, inabidi mtu asome dua ifuatayo
اَللّٰهُمَّ سَلِّمْنِيْ لِرَمَضَانَ وَسَلِّمْ رَمَضَانَ لِيْ وَسَلِّمْهُ لِيْ مُتَقَبَّلًا
ewe Allah! Nilinde kwa ajili ya ramadhaani, (kwa kunifanya nishuhudie mwezi wa ramadhaani nikiwa na afya na nguvu ili niweze kuchukuwa faida kamili ndani yake,) na nilindie mwezi wa ramadhaani (kwa kufanya ndani yake nipate faida kamili) na unikubalie.
عن عبادة بن الصامت قال: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يعلمنا هؤلاء الكلمات إذا جاء رمضان اللهم سلمني لرمضان وسلم رمضان لي وسلمه لي متقبلا.(الدعاء للطبراني، الرقم: 913)
Ubaadah Bin Saamit (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa anawafundisha maswahaba dua ifuatayo pindi ambapo inapokaribia ramadhaani.
اَللّٰهُمَّ سَلِّمْنِيْ لِرَمَضَانَ وَسَلِّمْ رَمَضَانَ لِيْ وَسَلِّمْهُ لِيْ مُتَقَبَّلًا
9. Kuwa na tabia ya kufanya matendo mema katika mwezi wa ramadhaani na uwache tabia ya kufanya matendo mabaya na madhambi.
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه و سلم إذا كان أول ليلة من شهر رمضان صفدت الشياطين ومردة الجن وغلقت أبواب النار فلم يفتح منها باب وفتحت أبواب الجنة فلم يغلق منها باب وينادي مناد يا باغي الخير أقبل ويا باغي الشر أقصر ولله عتقاء من النار وذلك كل ليلة (سنن الترمذي، الرقم: ٦٨٢)
Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema “pindi usiku wa kwanza wa ramadhaani unapoingia, mashetani na majini mabaya wanafungiwa, milango ya jahannamu inafungwa na amna mlango utakao funguliwa baada ya hapo (ndani ya mwezi wa ramadhaani,) milango ya pepo inafunguliwa amna mlango utakao fungwa baada ya hapo (ndani ya ramadhaani) na mtu atatangaza, ewe mwenye kutafuta uchamungu na mazuri, nenda mbele! Ewe mwenye kutafuta mabaya, jiepushe (na mabaya yako)! Na Allah subhaana wata’alah anawaacha watu wengi huru kutoka kwenye moto wa jahannam, na hii inatokea kila usiku wa ramadhaani nzima.”
10. Kama unauwezo wa kuandaa futari kwa mtu aliyefunga, inabidi ufanye hivyo, hata kama ni kumpa tende moja kwa ajili ya kufungulia swaumu.
عن زيد بن خالد الجهني قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من فطر صائما كان له مثل أجره غير أنه لا ينقص من أجر الصائم شيئا (سنن الترمذي، الرقم: ٨٠٧، وقال: هذا حديث حسن صحيح)
Sayyidina Zaid Bin (radhiyallahu ‘anhu) Khaalid Al-juhani ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “mtu ambaye ana andaa futari kwa aliyefunga, atapata thawabu sawa sawa na yeye (mwenye aliyefunga) bila ya thawabu ya aliyefunga kupungua kwa njia yoyote).
11. Tumia muda wako kukaa na wachamungu wa Allah Ta’ala ili upate faida kamili katika mwezi huu.
12. Jiepushe na kitu chochote cha haramu au chenye mashaka, iwe chakula cha mashaka, matendo ya mashaka na kauli za mashaka n.k
13. Kufunga katika mwezi wa ramadhaani ni ibada kubwa. Kwahiyo, wakati umefunga, hakikisha haujiusishi na matendo yoyote mabaya yatakayosababisha thawabu ya swaumu kupotea. Vile vile, mtu ajiepushe kuhusiana na mambo yoyote yasiyo muhimu wakati anapofunga (kwa mf kuongea upuuzi,matendo yenyehayana faida n.k)
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه و سلم رب صائم ليس له من صيامه إلا الجوع ورب قائم ليس له من قيامه إلا السهر (سنن ابن ماجة، الرقم: ١٦٩٠)
Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema “wapo wengi waliofunga, lakini hawapati kitu kwa swaumu zao isipokuwa kushinda na njaa, na wapo wengi wanaoswali usiku lakini hawapati kitu, isipokuwa kujisumbuwa kukaa macho tu usiku)
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : من لم يدع قول الزور والعمل به فليس لله حاجة في أن يدع طعامه وشرابه (صحيح البخاري، الرقم: ١٩٠٣)
Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema ” yoyote asiejiepusha na maneno na matendo mabaya (ndani ya swaumu), Allah Ta’ala ahitaji yeye kutokunywa na kula kwake).
14. Ukiwa umefunga, jiepushe na ubishi na kupigana. Kama mtu anataka kubishana na mtu aliyefunga, inabidi amuambie kwa adabu,’ kwamba mimi nimefunga” (yaani aimpendezi mwenye kufunga aingie kwenye ugomvi, kupigana na kubishana)
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : وإذا كان يوم صوم أحدكم فلا يرفث ولا يصخب فإن سابه أحد أو قاتله فليقل إني امرؤ صائم (صحيح البخاري، الرقم: ١٩٠٤)
Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema kwamba “pindi mmoja wenu amefunga, asijishughulishe na kuongea machafu, na kufoka na kupiga kelele. Kama mtu anamdhulumu mwenye kufunga au anapigana nae, basi aseme (kwa adabu) mimi nimefunga”.