عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من ذكرت عنده فليصل علي فإنه من صلى علي مرة صلي عليه عشرا (المعجم الأوسط للطبراني، الرقم: 2767، ورجاله رجال الصحيح كما في القول البديع صـ 237)
Anas Bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “mtu ambae jina langu limetajwa mbele yake anatakiwa atume salamu juu yangu, na kwa hakika yoyote ambae ananitumia salamu mara moja, Allah subhaana wata’alah atamtumia baraka kumi juu yake.”
Kuheshimiwa na Allah subhaana wata’alah Kwa sababu ya kumswalia Nabi wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa wingi.
Imeripotiwa kuhusu Abul Abbaas, Ahmed Bin Mansoor (rahimahullah), kwamba baada ya yeye kufariki, mtu kutoka kwa wenyeji wa Sheeraaz alimuona kwenya ndoto. Ndani ya ndoto, Ahmed Bin Mansoor alikuwa anasimama ndani ya mihraab ya msikiti mkuu wa sheeraaz. Alikuwa amepambwa na seti ya mavazi (mazuri) na alikuwa na taji kichwani lilopambwa na mawe ya thamani.
Ule mtu alimuuliza,” ni jinsi gani Allah subhaana wata’alah alikushughulikia?” alijibu,” Allah subhaana wata’alah alinisamehe madhambi yangu, akanipa heshima, akanivisha taji la jannah na akanibarikia kwa kuingia jannah”. Kisha mtu akaulizwa, ” kupitia kitendo gani Allah subhaana wata’alah alikuheshimu kwa nafasi hii ya juu?” akajibu, ” kwa sababu ya salamu nyingi ambazo nilikuwa namswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam). (Al-Qawlul Badee Pg.259)