Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 3

15. Kwenye mwezi wa ramadhaani, jaribu kuzidisha kwa wingi matendo mazuri. Imepokelewa katika hadith kwamba ibada yoyote ile ya nafili (matendo mazuri ya hiyari) yaliyofanyika katika mwezi wa ramadhaani, inamchumia mtu thawabu ya kitendo cha faradhi, na thawabu ya kitendo cha faradhi kilicho fanyika katika mwezi wa ramadhaani kinazidishwa mara sabini

عن سلمان رضي الله عنه قال خطبنا رسول الله صلى الله عليه و سلم في آخر يوم من شعبان … من تقرب فيه بخصلة من الخير كان كمن أدى فريضة فيما سواه ومن أدى فريضة فيه كان كمن أدى سبعين فريضة فيما سواه (الترغيب والترهيب، الرقم: ١٤٨٣)

Sayyidina Salmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alitoa khutuba siku ya mwisho ya shaabani (ambamo amesema) “mtu mwenye kumkaribia Allah ta’ala kwakufanya kitendo cha nafili chochote, atapata thawabu sawa sawa na yule ambaye alifanya kitendo cha faradhi muda mwingine wowote ule. Mtu anayefanya kitendo cha faradhi katika mwezi huu atabarikiwa na thawabu ya yule ambaye anafanya faradhi sabini kwa muda mwingine wowote ule.”

16. Hakikisha unaswali rakaah ishirini za tarawehe kila usiku. Swala ya tarawehe ni sunna iliyosisitizwa. Kwenye zama za Sayyidina Umar (radhiyallahu ‘anhu), maswahaba wote (radhiyallahu ‘anhum) walikuwa na makubaliano ya kuswali rakaa ishirini za tarawehe. Jitahidi angalau umalize qur an nzima kwenye swala ya tarawehe.

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : من قام رمضان إيمانا واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه (صحيح البخاري، الرقم: ٣٧)

Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema “yoyote anayesimama kwenye tarawehe katika ramadhaani akiwa na iman ( kuamini kwa ukamilifu) na akiwa anatarajia malipo, madhambi yake yote yaliyopita ( dhambi ndogo ndogo) yatasamehewa.”

عن عبد الرحمن بن عوف رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إن الله تبارك وتعالى فرض صيام رمضان عليكم وسننت لكم قيامه فمن صامه وقامه إيمانا واحتسابا خرج من ذنوبه كيوم ولدته أمه (سنن النسائي، الرقم: ٢٢١٠)

Sayyidina Abdur Rahman Bin Auf (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “hakika Allah subhaana wata’alah amefaradhisha swaumu ya ramadhaani juu yenu na nimewaamrisha kusimama usiku wake (kwenye swala ya tarawehe). Yoyote ambaye anafunga mchana na anasimama usiku kwenye swaala ya tarawehe na imani ya kweli na anatarajia thawabu kutoka kwa Allah subhaana wata’alah madhambi yake yote yatasafishwa kama siku ambayo mama yake alimzaa.”

عن أبى الحسناء أن علي بن أبي طالب أمر رجلا أن يصلي بالناس خمس ترويحات عشرين ركعة – باب ما روي في عدد ركعات القيام في شهر رمضان (السنن الكبرى للبيهقي، الرقم: ٤٨٠٥)

Abul Hasnaa (rahimahullah) amesema, “Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu) alimchaguwa mtu kuwaswalisha watu rakaa ishirini za tarawehe kwenye ramadhaani.

عن الأعمش عن زيد بن وهب قال كان عبد الله بن مسعود يصلي لنا في شهر رمضان فينصرف عليه ليل قال الأعمش كان يصلي عشرين ركعة و يوتر بثلاث (عمدة القاري ١١/١٢٧)

A’amash (rahimahullah) amesema, kwenye mwezi wa ramadhaani, Sayyidina Abdullah Bin Mas’ood (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa-anawaswalisha watu kwenye swala ya tarawehe. Alikuwa naswali rakaa ishirini za tarawehe na rakaa tatu za witri.”

روى البيهقي بإسناد صحيح انهم كانوا يقيمون على عهد عمر بعشرين ركعة وعلى عهد عثمان وعلي (عمدة القاري ٥/٢٦٧)

Allamah Ayni (rahimahullah) amesema, “maswahaba wa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) walikuwa wanaswali rakaa ishirini za tarawehe kwenye zama za Sayyidina Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) na Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu).”

17. Zidisha matendo manne katika ramadhaani:

(A) kisomo cha kalima ‘laa ilaaha illallah’

(B) istighfaar

(C) kuomba kuingizwa peponi

(D) kuomba kukingwa na moto wa jahannam

عن سلمان رضي الله عنه قال خطبنا رسول الله صلى الله عليه و سلم في آخر يوم من شعبان… واستكثروا فيه من أربع خصال خصلتين ترضون بهما ربكم وخصلتين لا غناء بكم عنهما فأما الخصلتان اللتان ترضون بهما ربكم فشهادة أن لا إله إلا الله وتستغفرونه وأما الخصلتان اللتان لا غناء بكم عنهما فتسألون الله الجنة وتعوذون به من النار (صحيح ابن خزيمة، الرقم: ١٨٨٧)

Sayyidina Salmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alitoa khutuba kwenye siku ya mwisho ya shaabani (ndani mwake alisema), “na (katika mwezi huu) fanya matendi manne kwa wingi. Matendo mawili ni ya kumridhizisha mola wenu na matendo mawili ambayo uwezi kuishi bila ya kuyafanya. Matendo mawili ya kumridhisha Allah ni kusoma kalima ya “laa ilaaha illallah” na kuomba msamaha wake. Na matendo mawili ambayo huwezi kuya acha ni kumuomba Allah subhaana wata’alah kuingizwa peponi, na kuomba akuepushe na moto wa jahannam.”

18. Fanya dua kwa wingi ndani ya ramadhaani. Dua ya mtu aliye funga inakubalika, haswa dua iliyofanywa kabla ya kufuturu.

عن أبي هريرة قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ثلاثة لا ترد دعوتهم الصائم حتى يفطر والإمام العادل ودعوة المظلوم يرفعها الله فوق الغمام ويفتح لها أبواب السماء ويقول الرب وعزتي لأنصرنك ولو بعد حين (سنن الترمذي، الرقم: ٣٥٩٨)

Sayyidina Abuu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema “kuna watu watatu dua zao hazikataliki, mtu aliyefunga mpaka atakapo funguwa swaumu yake, kiongozi muadilifu, na mtu aliyedhulumiwa Allah subhaana wata’alah anainuwa dua zao juu ya mawingu na anafunguwa milango ya mbingu. Allah subhaana wata’alah akisema naapa juu ya utukufu wangu kwa hakika nitakusaidia, hata kama itakuwa baada ya muda.

عن عمرو بن شعيب عن أبيه عن جده قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول للصائم عند إفطاره دعوة مستجابة وكان عبد الله بن عمرو إذا أفطر دعا أهله وولده ودعا (شعب الايمان، الرقم: ٣٦٢٤)

Sayyidina Abdullah Bin Amr (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema ” muda wa kufuturu, dua ya mtu aliyefunga inakubalika. “Kwa hivyo” Abdullah Bin Amr (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa anaita familia yake na watoto wake wakati wa kufuturu na wakiomba dua.

19. Mwezi wa ramadhaani unajulikana kuwa ni mwezi wa qur’an. Kwahiyo, mtu asome qur’an kwa uwezekanavyo. Yule aliyehifadhi asome zaidi kuliko yule ambae ajahifadhi.

20. Kuwa mkarimu ndani ya mwezi wa ramadhaani. Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa anaonyesha ukarimu sana ndani ya mwezi wa ramadhaani kuliko miezi mingine.

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال كان رسول الله صلى الله عليه وسلم أجود الناس وكان أجود ما يكون في رمضان حين يلقاه جبريل وكان يلقاه في كل ليلة من رمضان فيدارسه القرآن فلرسول الله صلى الله عليه وسلم أجود بالخير من الريح المرسلة (صحيح البخاري، الرقم: 6)

Sayyidina Ibun Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa mkarimu sana miongoni mwa watu. Alifika kwenye kiwango cha juu cha ukarimu katika mwezi wa ramadhaani pindi Sayyidina jibra’eel (alahis salaam) alipokuwa anakuja kumuona “kufanya murajaa wa qur’an tukufu” Sayyidina Jibre’eel (alahis salaam) alikuwa anakuja kumuona kila usiku wa ramadhaani ambapo walikuwa wanasomeana qur’an tukufu. Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa mkarimu zaidi ya upepo wenye faida ukiwa unavuma (yaani upepo unajulikana kuwa hauna mwisho na unafika sehemu zote, kwahiyo ukarimu wa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ulipita zaidi ya upepo kuonyesha viumbe mapenzi.

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa …