4. Baada ya kumaliza kula, kwanza ondoa chakula kwenye mkeka kabla ya kuamka na kuondoka. Wakati wa kuondoka, Dua ifuatayo inapaswa kusomwa:
اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ حَمْدًا كَثِيْرًا طَيِّبًا مُبَارَكًا فِيْهِ غَيْرَ مَكْفِيٍّ وَلَا مُوَدَّعٍ وَلَا مُسْتَغْنًى عَنْهُ رَبَّنَا
Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala), sifa kama hizo ambazo ni nyingi, safi na kamili kwa baraka. Ee Mola wetu, hatuhesabu sifa zetu kutosheleza (kwa chakula ambacho umetupa), wala hatuchukui Sifa zetu kuwa sifa ya mwisho (kwa kile umetupatia), na wala hatujifikirii kuwa huru (wa Kukusifu kwa yote ambayo umetupa).
5. Baada ya kula, safisha mikono na usukutuwe mdomo.
Sunna na Adabu za kula
1. Usikosowi au kutafuta kosa na chakula.
Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) hakuwahi kutafuta kosa na chakula. Ikiwa alitaka kula, alikula, na ikiwa hakuwa na hamu ya kula, aliiacha (bila kutafuta kosa nacho).
2. Usile chakula cha moto sana.
Asmaa bint abi bakr (Radhiyallahu anha) anasimulia kwamba kila alipopewa thareed (aina flani ya chakula), angeamuru kwamba ifunikwa hadi moto lipunguwe kidogo (na ikawa rahisi kula). Angesema, “Nilimsikia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akisema kwamba (kula chakula ambacho sio moto sana) ni chanzo cha baraka nyingi. “
3. Kutokuharibu chakula na kutokuwa na israaf kwenye chakula na vinywaji.
Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) katika Quraan Majeed anasema, “Kula na kunywa, na usifanyi israaf, hakika yeye (Mwenyezi Mungu subhaanahu wata’ala) hapendi wale ambao wanafanya israaf.
Abdullah bin amr bin aas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Kula, kunywa na toa sadaqa na vaa nguo nzuri, kama tu hakuna kiburi.”