Abu Hurairah (Radhiyallahu ‘Anhu) anaripoti kwamba wakati moja, baada ya swala alfajiri, Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) alimwambia Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu), “Ewe Bilaal! Kutoka kwa vitendo unavyofanya za kiislam, niambie ni kitendo gani unachokifanya kikubwa la kukufaidisha Akhera, kwa sababu usiku wa jana, nilikuwa nimesikia nyayo zako mbele yangu huko Jannah (ndani ya ndoto ambayo nilikuwa nimeona). ”
Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) akajibu, “Kitendo ninachokifanya, ambacho natumai kitaninufaisha sana, ni kwamba wakati wowote ninapofanya Wudhu, wakati wowote mchana au usiku, nakuwa naswali baada ya kufanya wudhu (yaani naswali Tahiyyatul wudhu). “(Muslim #2458)
Katika Hadith hii, tunaona kwamba kwa sababu ya kuswali Tahiyyatul Wudhu, Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alibarikiwa na heshima ya kuwa na Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) huko Jannah katika ndoto alionyeshwa. Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) kutembea mbele ya Rasulullah (Sallallahu Alaihi Wasallam) inalenganishwa na Khaadim (mtumishi) anayetembea mbele ya mfalme wake ili kumhudumia na kuangalia usalama wake.