Kupata dua maluum ya wamalaikah

عن عامر بن ربيعة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه و سلم قال: ما من مسلم يصلي علي إلا صلت عليه الملائكة ما صلى علي فليقلَّ العبد من ذلك أو ليكثر (سنن ابن ماجة، الرقم: ٩٠٧، وإسناده ضعيف كما في مصباح الزجاجة ١١٢/١)

Aamir bin Rabee’ah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabiii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “yoyote atakae niswalia, wamalaikah wataendelea kumswalia yeye (yaani: kumuombea dua) kama ataendelea kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Kwa hiyo, imebaki kwa mtu kuamua kama atataka kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) kidogo au kwa wingi.”

Salamu kuja kumsaidia mtu wakati wa shida

Sheikh Shibli (rahimahullah) ameripoti qissa kifuatacho:

Wakati mmoja, moja wa majirani zangu alifariki. Baada ya muda flani, nilimuona kwenye ndoto. Nikamuuliza,” jinsi gani Allah subhaana wata’alah alikushughulikiya?” akajibu:

“Ewe Shibli! Nilipata misukosuko na shida nyingi, kwa sababu nilikuwa sina uwezo wa kujibu maswali ya wamalaikah kaburini! Pindi niligunduwa kama sina uwezo wakuongea na kujibu, nikajifikiria, kwanini na pata hizi misukosuko? Kwani sikufa na imani? wakati hii fikra ilinijia akilini, kuna sauti iliniita, hii ni adhabu yako kwa sababu ya wewe kuwa ghafili wakati wakutumia ulimi wako duniyani.

“Baada ya hapo, wakati wamalaikah wawili walitaka kumuadhibu, mtu mwenyewe alikuwa mzuri sana na alikuwa anatowa harufu nzuri alikuja katikati ya mimi na wamalaikah na akanisaidia kujibu maswali vizuri. Baada ya mimi kujibu maswali vizuri na kuepuka na adhabu, nilimuuliza ule mtu,’ wewe ni nani? Allah awe na rehma juu yako! ule mtu akajibu, mimi ni mtu aliye umbwa na Allah kupitia salamu nyingi zenye ulikuwa unamtumia nabi wa Allah Mimi nimetumwa na nimeamrishwa kukusaidia wakati wa shida zako.” (Al-Qawlul Badee, Pg,265)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …