Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 4

21. Kuna baraka nyingi kwa kuamka muda wa daku. Kwa hiyo mtu atimize sunna ya daku kabla kuanza kufunga.

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم السحور كله بركة فلا تدعوه ولو أن يجرع أحدكم جرعة من ماء فإن الله عز و جل وملائكته يصلون على المتسحرين رواه أحمد وإسناده قوي (الترغيب والترهيب، الرقم: ١٦٢٣)

Sayyidina Abuu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema daku inabaraka nyingi. Kwahiyo usiache sunna ya daku, hata kama mtu anaweza kunywa tonye moja la maji muda wa daku (inabidi mtu afanye hivyo ili atimize sunna ya daku.) Kwa hakika Allah subhaana wata’alah ananyunyizia rehema zake maalumu juu ya wale ambao wanaamka muda wa daku na malaika wanawaombea dua maalumu).

وعن عمرو بن العاص رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم فصل ما بين صيامنا وصيام أهل الكتاب أكلة السحر. (صحيح مسلم، الرقم: ١٠٩٦)

Sayyidina Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “tofauti ya swaumu zetu na ahl ul kitaab (watu waliyopita) ni kula daku.”

22. Muda wa daku unaanza kuanzia usiku wa manane. Lakini ni vizuri kuchelewesha daku mpaka muda wa mwisho wa daku, kabla ya swaumu kuanza (yaani kabla ya alfajiri ya kweli kuanza) mbali ya hapo mtu asicheleweshe sana mpaka kuna khofu ya kupitiliza muda.

عن أنس بن مالك رضي الله عنه أن نبي الله صلى الله عليه وسلم وزيد بن ثابت تسحرا فلما فرغا من سحورهما قام نبي الله صلى الله عليه وسلم إلى الصلاة فصلى قلنا لأنس كم كان بين فراغهما من سحورهما ودخولهما في الصلاة قال قدر ما يقرأ الرجل خمسين آية (صحيح البخاري، الرقم: ٥٧٦)

Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na Sayyidina Zaid Bin Thabit (radhiyallahu ‘anhu) walikaa ili wale daku. Pindi walipomaliza daku, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisimama kwa ajili ya kuswali alfajr. Wafuasi wa Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) walimuuliza, “kwa muda gani baada ya kumaliza daku mpaka muda waliyoswali alfajiri? Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) alijibu, “ule muda ulikuwa sawa sawa na muda unaomchukuwa mtu kusoma aya hamsini za qur an.”

23. Mtu akiamka muda wa daku, inabidi aswali tahajudi. Ramadhaani inampa mtu fursa nzuri ya kuanza kuswali tahajudi kwa sababu yupo macho muda wa daku.

24. Jua likizama tu mtu aanze kufuturu( afungue swaumu yake) baada ya kuzama kwa jua.

عن سهل رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : لا يزال الناس بخير ما عجلوا الفطر. قال أبو عيسى حديث سهل بن سعد حديث حسن صحيح (سنن الترمذي، الرقم: ٦٩٩)

Sayyidina Sahl (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “watu watabaki kwenye uzuri kama wataharakisha kufungua swaumu zao.”

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم قال الله تعالى أحب عبادي إلي أعجلهم فطرا. (سنن الترمذي، الرقم: ٧٠٠)

Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema kama Allah subhaana wata’alah amesema, “watu ambao wamependwa sana na mimi niwale ambao wanao harakisha kufungua swaumu zao muda wa kufuturu.”

25. Ni bora zaidi mtu afungue swaumu yake kwa tende na maji.

عن سلمان بن عامر قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا أفطر أحدكم فليفطر على تمر فإنه بركة فإن لم يجد تمرا فالماء فإنه طهور (سنن الترمذي، الرقم: ٦٥٨)

Sayyidina Salmaan Bin Aamir (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “muda wa kufuturu, mtu afungue swaumu yake na tende kwa sababu imejaa baraka, na kama mtu hana tende, basi anywe maji hiii ni njia iliyosafishika.”

عن أنس قال : كان النبي صلى الله عليه وسلم يفطر قبل أن يصلي على رطبات فإن لم تكن فتميرات فإن لم تكن تميرات حسى حسوات من ماء (سنن الترمذي، الرقم: ٦٩٦)

Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa anafunguwa swaumu yake na tende za fresh kabla ya kuanza kuswali magharib. Kama tende za fresh hazikupatikana, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa anafungua swaumu yake na tende iliyo kavu. Kama tende kavu hazikupatikana, basi Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa anafunguwa swaumu yake na maji.

26. Inabidi mtu asome dua ifuatayo wakati wa kufuturu:

اَللّهُمَّ لَكَ صُمْتُ وَعَلى رِزْقِكَ أَفْطَرْتُ فَتَقَبَّلْ مِنِّيْ إِنَّكَ أَنْتَ السَّمِيعُ العَلِيم

Ewe Allah! nimefunga hii swaumu kwa ajili yako tu, na kupitia rizqi yako nimefungua swaumu yangu, basi nikubalie swaumu. Kwa hakika wewe ni mwenye kusikia kila kitu na mwenye kujua kila kitu.

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوْقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللّٰهُ

Kiu changu kimekwisha na mishipa yangu imefunguka na thawabu imepatikana (kutoka kwa allah) inshaa allah.

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …