عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال من صلى علي عشرا صلى الله عليه مئة ومن صلى علي مئة صلى الله عليه ألفا ومن زاد صبابة وشوقا كنت له شفيعا وشهيدا يوم القيامة (أخرجه أبو موسى المديني بسند قال الشيخ مغلطاى لا بأس به، كذا في القول البديع صـ ٢٣٦)
Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) amesema “yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara kumi, Allah subhaana wata’alah atatuma salaam kwake mara mia moja, na yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara mia moja, Allah subhaana wata’alah atamtumia salaam kwake mara elfu moja, na yoyote atakaye zidisha (kunisalia mimi) kwa ajili ya upendo (kwa ajili yangu) na kwa hamu (kwa ajili ya kutafuta thawabu), nitamuombea na nitakuwa shahidi kwa ajili yake siku ya mwisho”.
Kusaidiwa Kwa Adhabu Kwa Sababu Ya Kumsalia Nabii Mara Nyingi
Siku moja mtu aliona mtu kwenye ndoto yake yenye kutisha sana na yenye fomu ya kutisha. Kwa kumuulizia ule mtu kama yeye ni nani, ule mtu alijibu, “mimi ni mabaya yako.”Kisha alimuuliza, “nawezaje kuokolewa kutoka kwako? “Alijibu, “kwa kuendelea kumswalia Nabii wa Allah mara nyingi.” (Al-Qawlul Badee, Pg.168)