Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 5

27. Kaa kwenye itikafu siku 10 za mwisho za ramadhaani kama unauwezo.

عن ابن عباس الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال في المعتكف هو يعتكف الذنوب ويجري له من الحسنات كعامل الحسنات كلها (سنن ابن ماجة، الرقم: ٢١٠٨)

Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema kuhusu mwenye kukaa itkafu, “mwenye kukaa itkafu (ndani ya msikiti) anajiepusha na madhambi, na kwa wakati wote, anapata thawabu ya kufanya ibada mbali mbali angekuwa na uwezo wa kuzifanya kama asingekuwa kwenye itkafu”.

عن ابن عباس الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال من اعتكف يوما ابتغاء وجه الله تعالى جعل الله بينه وبين النار ثلاث خنادق أبعد مما بين الخافقين رواه الطبراني في الأوسط والبيهقي واللفظ له (الترغيب والترهيب الرقم: ١٦٥٠)

Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema” yoyote atakae kaa kwenye itkafu kwa siku moja kwa ajili ya kuomba radhi za Allah, kati ya yeye na moto wa jahannam Allah subhaana wata’alah ataweka mifereji mitatu, kwa kila mfereji mmoja una upana kutoka mashariki mpaka magharib”

28. Tafuta usiku wa laila tul qadr katika usiku zisizo gawanyika katika siku kumi za mwisho za ramadhaani.

عن أنس بن مالك قال: دخل رمضان فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إن هذا الشهر قد حضركم وفيه ليلة خير من ألف شهر من حرمها فقد حرم الخير كله ولا يحرم خيرها إلا محروم (سنن ابن ماجه، الرقم: ١٦٤٤)

Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba pindi mwezi wa ramadhaani ulipo anza, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema “kwa hakika huu mwezi (wa ramadhaani) umefika juu yenu, na ndani yake kuna usiku bora kuliko miezi elfu moja. Mwenye kuukosa huu usiku kwa hakika atakuwa amekosa uzuri wote na mwenye kukosa ni wale ambao waliokosa uzuri wa huu usiku.

29. Kwenye siku zisizogawanyika, zidisha ibada zako. Pindi unapoenda kulala, Weka nia ya kuamka baadae usiku kufanya ibada zaidi. Jaribu kufanya ibada kabla ya kulala, kwa sababu kuna uwezekano ya wewe kutokuamka baadae ili ufanye ibada.

30. Kwenye usiku wa lalatul qadr, soma dua ifuatayo:

اَللّٰهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّيْ

Ewe Allah! kwa hakika wewe ni mwenye kusamehe unapenda kusamehe, basi nakuomba unisamehe.

عن عائشة قالت: قلت يا رسول الله أرأيت إن علمت أي ليلة ليلة القدر ما أقول فيها ؟ قال قولي اللهم إنك عفو تحب العفو فاعف عني قال هذا حديث حسن صحيح (سنن الترمذي، الرقم: ٣٥١٣)

Sayyidatuna Aaisha (radhiyallahu ‘anha) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, alimuuliza Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) dua gani asome kama akipata usiku wa lalatul qadr. Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimfundisha kusoma dua ifuatayo:

اَللّٰهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّيْ

31. Yoyote ambaye anaswali isha na swala ya alfajir kwa jamaah, na anaswali rakaa ishirini za tarawehe na imaam, Allah subhaana wata’alah atampa thawabu ya kusimama usiku mzima kwenye ibada, na kama usiku ulikuwa ni wa lalatul qadr, Allah ta’ala atampa thawabu ya lalatul qadr.

عن عثمان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى العشاء في جماعة فكأنما قام نصف الليل ومن صلى الصبح في جماعة فكأنما صلى الليل كله (صحيح مسلم، الرقم: ٦٥٦)

Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote atakae swali swala ya isha katika jamaah (katika msikitini) ni kama ametumia nusu ya usiku kwenye ibada, na yule ambae (ameswali swala ya isha kwenye msikiti katika jamaat na baada ya hapo) ameswali swala ya alfajir kwenye jamaah ( msikitini), Allah ta’ala atampa thawabu ya kutumia usiku mzima kwenye ibaada”

عن أبي ذر: قال … فقام بنا حتى ذهب ثلث الليل ثم لم يقم بنا في السادسة وقام بنا في الخامسة حتى ذهب شطر الليل فقلنا له يا رسول الله لو نفلتنا بقية ليلتنا هذه ؟ فقال إنه من قام مع الإمام حتى ينصرف كتب له قيام ليلة (سنن الترمذي، الرقم: ٨٠٦)

Sayyidina Abuu Zar (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti: kwenye usiku wa tarehe 25 katika ramadhaani, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alituswalisha kwenye swala ya tarawehe mpaka nusu ya usiku ulipita. (tulifurahia kuswali swala ya tarawehe mpaka) baada ya kumaliza kuswali, tulisema kwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) kama ungendelea mpaka mwisho wa usiku!” Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, yoyote anae simama na imaam na akaswali swala ya tarawehe, Allah ta’ala anamuandikia thawabu ya kusimama usiku mzima.

32. Kwenye usiku wa eid, tumia baadhi ya muda kwenye ibaada.

عن أبي أمامة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه و سلم قال من قام ليلتي العيدين محتسبا لم يمت قلبه يوم تموت القلوب رواه ابن ماجه ورواته ثقات إلا أن بقية مدلس وقد عنعنه (الترغيب والترهيب، الرقم: ١٦٥٥)

Sayyidina Abuu Humaamah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote atakae simama kwenye ibaada katika usiku za eid mbili na anatarajia kupata thawabu, roho yake aitakufa siku ambazo roho zitakufa.” (siku ambayo roho zitakufa inamaanisha muda wa fitna na fasaad wakati roho za watu zitampuuzia Allah subhaana wata’alah.Katika muda huo, Allah ta’ala ataiweka roho yake ikiwa hai kwa kumbukumbu.)

33. Baada ya mwezi wa ramadhaani, inatakiwa mtu ajitahidi kufunga sunna sita za swaumu ya shawwaal.

عن أبي أيوب الأنصاري أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : من صام رمضان ثم أتبعه ستا من شوال كان كصيام الدهر. (صحيح مسلم، الرقم: ١١٦٤)

Sayyidina Abuu Ayoob Ansaari (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote ambaye anafunga swaumu ya ramadhaani na akazifatisha kwa kufunga swaumu sita za shawwaal kisha (atapata thawabu) kama vile alifunga mwaka mzima.

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa …