عن جابر رضي لله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من صلى علي في كل يوم مائة مرة قضى الله له مائة حاجة سبعين منها لآخرته وثالثين منها لدنياه (أخرجه ابن منده وقال الحافظ أبو موسى المديني: إنه غريب حسن، كذا في القول البديع صـ ٢٧٧)
Hadrat Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Alisema, “yoyote atakae nitumia salaam mara mia moja kwa kila siku, Allah ta’ala atatimiza mahitaji zake mia, sabini za aakherah na thalathini za duniani.”
Kumswalia Nabii wa allah idaadi maalum kabla ya kulala
Sheikh ibnu Hajar Makki (rahimahullah) anaeleza kissa ya mchamungu ambae alijitolea kumswalia Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa idaadi maalum kabla ya kulala. Usiku moja, alimuona Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwenye ndoto. Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Aliingia nyumbani kwake na nyumba nzima ikajaa na nuru ya Nabii wa Allah. Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Akamwambia, “leta kwangu ule mdomo ambao unanitumiaga salaam na uniruhusu niubusu.”kutokana na aibu, aliweka mbele shavu yake na Nabii wa allah (sallallahu ‘alahi wasallam) akaibusu. Alivoamka, alikuta nyumba yake nzima inaharufu nzuri ya miski. (Ad-Durul Mandood, Pg.187)