Mahitaji yote ya dunia na ya deeni kutimizw

عن محمد بن يحي بن حبان عن أبيه عن جده حبان بن منقذ أن رجلا قال: يا رسول الله أجعل ثلث صلاتي عليك قال: نعم إن شئت قال الثلثين قال: نعم قال: فصلاتي كلها قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إذن يكفيك الله  ما أهمك من أمر دنياك وآخرتك (المعجم الكبرى للطبراني، الرقم: ٣٥٤٧ ،وإسناده حسن كما في الترغيب والترهيب للمنذري، الرقم: ٢٥٧٨)

Habbaan Bin Munqiz (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba sahabi moja aliwahi kumuuliza Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam), “Ewe mjumbe wa Allah (sallallahu alaih wasallam) je nijitolee thuluthi moja ya muda  ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? “Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alijibu, “ndio, kama utapenda.” Ule sahabah akauliza, “je nijitolee thuluthi mbili ya muda ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? “Nabii wa allah akajibu tena, “ndio, kama utapenda. “ule sahabah akauliza, “je nijitolee muda wote kukutumia salaam? “Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) akajibu, “kama utafanya hivyo, Allah subhaana wata’alah Atayatimiza mahitaji yako yote ambayo unayo (na amboyo ungeulizia kwenye dua yako), ikiwa niyakuhusu dunia au aakhera.”

Kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) wakati wa maumivu

Abdul Raheem Bin Abdul Rahmaan (rahimahullah) anasema: Siku moja, mkono wangu uliumia kwasababu ya kuanguka bafuni, na ulivimba vibaya sana. Ule usiku, maumivu yalisababisha usumbufu mwingi. Hatimaye, macho yangu yalifunga na nikalala kidogo. Katika maono, nilimuona Nabi wa allah (sallallahu alaih wasallam) na yote niliweza kusema ni, “ya Rasulullah (sallallahu alaih wasallam) “tuu.
Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) alinijibu, “kisomo chako kingi cha salaam kwa sababu ya maumivu kwenye mkono wako imenitia wasiwasi mwingi.” Wakati niliamka, nilikuta yale maumivu yamekwisha kabisa na uvimbe umeondoka. (Al-Qawlul Badee, Pg,341)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …