Heshima ya Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwa Maulamaa wakubwa.

Wakati mmoja, Zaid bin Thaabit (Radhiya Allaahu ‘anhu) alianza kupanda usafiri wake. Wakati Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alipomwona akipanda usafiri wake, alikimbia haraka, akashika kamba wa mnyama huyo na kumsaidia kupanda mnyama wake.

Kwa heshima ya Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma), Zaid (Radhiya Allaahu ´anhu) akamwambia na kusema: “Ewe binamu wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)! Usifanye hivyo (yaani. achilia kamba wa mnyama)

Hata hivyo, Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) aliendelea kushikilia kamba wa mnyama huyo na akamwambia: “Hivi ndivyo tulivyofunzwa (na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)) kufanya kwa Maulamaa wetu na wazee miongoni mwetu (yaani. tunapaswa kwenda nje ya njia yetu kuwaheshimu na kuwatumikia).

Kisha Zaid bin Thaabit (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia: “Nyoosha mkono wako.” Wakati Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) aliponyoosha mkono wake kuelekea kwake, Zaid bin Thaabit (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliinama mbele, akaushika mkono wa Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) na akaibusu na kusema: “Hivi ndivyo tulivyofunzwa kufanya na familia yenye heshima ya kipenzi chetu Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). (Taarikh Ibn Asaakir 19/326).

Kutokana na tukio hili, tunaona heshima ya hali ya juu ambayo Abdullah bin Abbaas ‎(Radhiyallahu anhuma) alimpa Zaid bin Thaabit (Radhiyallahu anhu) kwa vile alikuwa miongoni mwa Maulamaa wa Swahaabah.

Vile vile, Zaid bin Thaabit (Radhiya Allaahu anhu) alionyesha heshima kubwa kwa Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu anhuma), licha ya kuwa alikuwa mdogo kuliko yeye kiumri, kwa sababu Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu anhuma) ametoka kwenye familia iliyobarikiwa ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).

About admin

Check Also

Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) Akimsaidia Maskini Kumwozesha Binti Yake.

Siku moja, kundi la maQurraa (wale waliokuwa wataalamu wa kusoma Qur-aan Majeed) kutoka Basrah walimjia …