Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) Hayupo Tayari Kufanyiwa Opereshen Ya Macho Kwa Sababu Ya Kuathiri Swala Yake.

Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alipatwa na tatizo la jicho ambalo lilisababisha kutokwa na maji mfululizo. Daktari mmoja alimshauri akisema, “Matibabu yanawezekana ikiwa uko tayari kuchukua hadhari kwa kufanya sajdah juu ya ubao ulioinuliwa kwa muda wa siku tano, badala ya juu ya ardhi.”

Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) akajibu, “Siko tayari kwa hili, sitoswali hata rakaa moja kwa namna hii. Nimemsikia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akisema, ‘Mtu ambaye kaacha Swalaah moja kwa kusudi, atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyaamah hali ya kuwa Mwenyezi Mungu amemkasirikia.’”

Sheikh Moulana Muhammad Zakariyya (rahimahullah) alitaja kuhusu tukio hilo hapo juu:

Inajuzu, katika hali ya kipekee, kuswali kwa njia aliyoshauriwa na daktari na hili halitaingia kwenye onyo lililotajwa katika Hadith. Hata hivyo, Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa na bidii kubwa katika Swalah na kutokana na umuhimu waliouonyesha kwa maamrisho ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), sahaabi huyu Abdullah bin Abbaas (Radhiyallahu ‘anhuma) hakuwa tayari kufanyiwa matibabu hayo. Kwa hakika, Maswahaabah (Radhiyallahu ‘anhum) walikuwa wamejitayarisha kutoa muhanga wa dunia nzima kwa ajili ya Swalaah moja.

(Fadhail-ul-amaal. pg84)

About admin

Check Also

Abdullah bin Abbaas Akishinda pamoja na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) usiku ili ajifunze swalah ya Tahajjud ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)

Mjomba wake Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu), alitamani mtoto wake Abdullah bin …