6. Unapoingia mji uliokuwa unaelekea au mji wowote unaokusudia kukaa kwa muda fulani, basi soma dua ifuatayo mara tatu:
اَللّٰهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيْهِ
Ewe Mwenyezi Mungu, tubariki katika mahali hii.
Kisha some dua ifuatayo:
اَللّٰهُمَّ ارْزُقْنَا جَنَاهَا وَحَبِّبْنَا إِلٰى أَهْلِهَا وَحَبِّبْ صَالِحِيْ أَهْلِهَا إِلَيْنَا
Ewe Mwenyezi Mungu, tupe katika mazao yake, tujaalie tuwe vipenzi kwa watu wake na wafanye wachamungu wa watu wake wawe wapenzi kwetu.
Pia soma dua ifuatayo:
أَعُوْذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ
Natafuta ulinzi kupitia maneno makamilifu na yenye manufaa ya Allah (yaani majina na sifa zake) kutokana na shari (madhara) ya viumbe Vyake.
Kumbuka: Ubora wa kusoma dua hii ni kwamba hakuna ubaya utakaompata mtu hadi haondoke.
7. Unaposafiri na usiku unapoingia, soma dua ifuatayo kupata ulinzi:
يَا أَرْضُ رَبِّيْ وَرَبُّكِ اللهُ أَعُوْذُ بِاللهِ مِنْ شَرِّكِ وَشَرِّ مَا فِيْكِ وَشَرِّ مَا خَلَقَ فِيْكِ وَمِنْ شَرِّ مَا يَدِبُّ عَلَيْكِ وَأَعُوْذُ بِاللهِ مِنْ أَسَدٍ وَأَسْوَدْ وَمِنَ الْحَيَّةِ وَالْعَقْرَبِ وَمِنْ سَاكِنِ الْبَلَدِ وَمِنْ وَالِدٍ وَمَا وَلَدَ
Ewe ardhi! Mola wangu na Mola wako ni Mwenyezi Mungu. Najikinga kutoka Mwenyezi Mungu na maovu yako (madhara yanayotokana na ardhi k.m. matetemeko ya ardhi, kuzama ardhini, n.k.), na ubaya vilivyomo ndani yako (k.m. mimea yenye madhara, n.k.), na ubaya wa vile alivyoviumba ndani yako (k.m. wadudu waharibifu na viumbe vingine vyenye madhara), na ubaya wa kile kinachotambaa juu yako (yaani. na naomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu na simba, nyoka mweusi (aina ya nyoka hatari sana), na nyoka zote na nge, na wakazi wa ardhini (binadamu na majini), na kutoka kwa hao kinachozaa na kilicho zaliwa (yaani kutoka kwa wanadamu na mashetani, au kutoka kwa kila kiumbe kilichoumbwa kwa kuzaa).
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu