Dua Zinazohusiana na Kusafiri 2

4. Unapoanza safari, soma dua zifuatazo:

Dua Ya Kwanza

بِسْمِ اللهِ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ سُبْحَانَ الَّذِيْ سَخَّرَ لَنَا هٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِيْنَ  وَإِنَّا إِلٰى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُوْنَ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ اَللهُ أَكْبَرْ اَللهُ أَكْبَرْ اَللهُ أَكْبَرْ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ سُبْحَانَكَ اللّٰهُمَّ إِنِّيْ ظَلَمْتُ نَفْسِيْ فَاغْفِرْ لِيْ فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوْبَ إِلَّا أَنْتَ

Kwa jina la Allah Ta’ala. Sifa zote njema ni za Allah Ta’ala, Ametakasika Allah Ta‘ala ambaye amemtiisha mnyama huyu (au akaliweka gari hili chini ya udhibiti wetu) ingawa sisi hatukuweza kulidhibiti (bila ya msaada wake). Hakika sisi tutarejea kwa Mola wetu. Sifa njema zote ni za Allah Ta’ala. Sifa njema zote ni za Allah Ta’ala. Sifa njema zote ni za Allah Ta’ala. Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi. Allah Ta’ala ndiye kubwa zaidi. Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi. Hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah. (Ewe Mwenyezi Mungu) Wewe ni mtakatifu zaidi. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe, kwa sababu hakuna anayesamehe madhambi isipokuwa Wewe.

Dua Ya Pili

اَللهُ أَكْبَرُ اَللهُ أَكْبَرُ اَللهُ أَكْبَرُ سُبْحَانَ الَّذِيْ سَخَّرَ لَنَا هٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِيْنَ وَإِنَّا إِلٰى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُوْنَ اَللّٰهُمَّ إِنَّا نَسْأَلُكَ فِيْ سَفَرِنَا هٰذَا البِرَّ وَالتَّقْوٰى وَمِنَ الْعَمَلِ مَا تَرْضٰى اَللّٰهُمَّ هَوِّنْ عَلَيْنَا سَفَرَنَا هٰذَا وَاطْوِ عَنَّا بُعْدَهُ اَللّٰهُمَّ أَنْتَ الصَّاحِبُ فِيْ السَّفَرِ وَالْخَلِيْفَةُ فِيْ الْأَهْلِ اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِن وَعْثَاءِ السَّفَرِ وَكَآبَةِ الْمَنْظَرِ وَسُوْءِ الْمُنْقَلَبِ فِيْ الْمَالِ وَالْأَهْلِ وَالْوَلَدْ

Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa!Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa! Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa! Ametakasika Allah Ta‘ala ambaye amemtiisha mnyama huyu (au akaliweka gari hili chini ya udhibiti wetu) ingawa hatukuweza kulidhibiti (bila msaada Wake). Hakika sisi tutarejea kwa Mola wetu. Ewe Mwenyezi Mungu, tunakuomba utujaalie katika safari hii tawfeeq ya kuwa na uchamungu, taqwa na kutekeleza vitendo hivyo vinavyokupendeza. Ewe Mwenyezi Mungu, ifanyie wepesi safari hii na utukunjie ardhi (ili tuweze kumaliza umbali kwa muda mfupi). Ewe Allah Ta’ala, Wewe uwe mwenzangu katika safari hii na ubaki kuwa mlinzi juu ya familia yangu (katika kutokuwepo kwangu yaani naiweka familia yangu katika uangalizi wako maalum). Ewe Mwenyezi Mungu, naomba ulinzi Wako kutokana na matatizo ya safari, na hali zisizohitajika na hali zinazonijia, na (naomba ulinzi Wako) kurudi vibaya (yaani kushuhudia misiba nikirudi) kuhusiana na mali yangu, mke na watoto wangu.

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Kusafiri 5

19. Beba jagi na maji ili uweze kutumia choo na kufanya wudhu. Pia beba msala …