CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v80), default quality

Sunna Na Adabu Kusafiri 5

19. Beba jagi na maji ili uweze kutumia choo na kufanya wudhu. Pia beba msala ili uweze kuswali.

20. Ikiwa wewe ni dereva, basi hakikisha kwamba unaendesha kwa usalama. Hakikisha usiwe mzembe katika uendeshaji wako.

21. Kuwa na taarifa zote muhimu za kibinafsi, na pia vitambulisho ambazo utavihitaji kwenye safari yako (k.m.
pasipoti, kitambulisho. nk).

22. Tafuta njia kabla ya kuanza safari.

23. Unapotumia choo au bafu mahali popote, basi hakikisha umeacha sehemu hiyo katika hali ya usafi. Usiiache katika hali ya uchafu kwa sababu itawasumbua wengine.

24. Unapopanda mahali popote, soma takbira (الله اكبر), na unaposhuka, soma tasbihi (سبحان الله).

Jaabir (Radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba Maswahaba walikuwa wakisoma takbira wakati wakipanda sehemu, na kusoma tasbihi wakati wa kushuka sehemu.

About admin

Check Also

Dua za Sunnah Wakati wa Kuamka

Dua Ya Kwanza اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا وَإِلَيْهِ النُّشُوْرْ Sifa njema zote …