Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) Akiwakirimu Wageni

Abaan bin Uthmaan (rahimahullah) anataja:

Wakati fulani, mtu fulani alifanya mpango wa kumsumbua Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) na kumletea sifa mbaya. Alikwenda kwa viongozi wote wa Maquraish na kuwaambia kwamba Ibnu Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) amewaalika kwenye chakula asubuhi iliyofuata. Mtu huyo alikwenda sehemu mbalimbali na akaendelea kuwaalika watu kwa niaba ya Abdullah bin Abbas (Radhiyallahu ‘anhuma).

Siku iliyofuata, wakati wa chakula, idadi kubwa ya watu walikusanyika nyumbani kwa Ibnu Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma), ambaye baada ya kupata ukweli wa jambo hilo, akawaomba watu wakae, akaanda matunda kutoka sokoni na akawakaribisha kula. Wakati Ibnu Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) akikaa nao na kuanza kuzungumza nao, idadi kubwa ya wapishi walianza kuandaa chakula kwa ajili ya wageni.

Walikuwa bado wanafurahia matunda wakati chakula chao kilikuwa tayari na kuandaliwa. Wageni wote walipomaliza kula na kushiba, Ibnu Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alimuuliza mweka hazina wake, “Je, tunaweza kumudu kuwaandalia watu vyakula hivyo kila siku?” Mweka hazina aliposema kuwa anaweza kumudu, Ibnu Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) aliwaambia watu, “Nyinyi wote mmealikwa kula chakula namimi kwa namna hii kila asubuhi.”

Maelezo:

Tukio hili lilitokea wakati ambapo Maswahabah (Radhiyallahu ‘anhum) walikuwa wameshinda vita vingi (na mali ya dunia ilikuwa mikononi mwao). Lakini, Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walitumia kwa ukarimu kiasi kwamba hawakuweka chochote kwao. Kuhusiana na mali, walikuwa kama ungo – maji yanapojazwa kwenye ungo, mara moja hutoka mpaka hakuna kitu kinachobaki.

Sahaabi angekuja kumiliki mali nyingi, kwa matokeo ya kutekwa, lakini kisha angegawa kila kitu alichokuwa nacho, na asibaki na dirham moja kwa ajili ya chakula.

Hawakuwa na mazoea ya kuhodhi pesa, wala kuwekeza chochote kwa ajili ya mahitaji yao ya baadaye. Mamia ya maelfu ya dirham, sehemu yao ya ngawira, zote walizigawa ndani ya dakika. (Fazail-ul-Sadaqat. kurasa 705)

About admin

Check Also

Elimu Kuu ya Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma)

Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anasema: Baada ya kifo cha Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), …