15. Wakati wa safari, ikiwa kuna hali ya usumbufu imejitokeza, basi fanya subira. Usikasirike wala usiwe mfidhuli, na hivyo kusababisha maumivu na usumbufu kwa wengine.
16. Tumia mbinu ya upole unaposhughulika na swahiba zako na kushiriki katika majadiliano ya urafiki na kucheka safarini. Usichukue mbinu ya kuwa mkali.
17. Usifunge safari bila ya kuwa ya lazima. Ikiwa una hitaji, basi nenda, na ukitimiza haja yako basi fanya haraka kurudi nyumbani.
Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anasema kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Kusafiri ni kama sehemu ya Jahannum ambayo humzuia mtu asipate chakula chake, kinywaji na usingizi wake (yaani, kusafiri kunaleta shida, kama vile mtu anavyopata shida katika Jahannum). Hivyo, mtu anapomaliza kusudi na kazi ya safari, anapaswa kuharakisha kurudi kwa familia yake.”
18. Unaposafiri, linda macho yako, na iwezekanavyo, jaribu kuepuka kukaa karibu na wanawake. Epuka kuzungumza na wahudumu wanawake au wasio Mahram. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) ametaja katika Qur-aan Majeed:
Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, hilo litakuwa safi zaidi kwao. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayoyafanya.
Ma’qil bin Yasaar (Radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Ni bora kwako wewe kuchomwa na sindano ya chuma kichwani kuliko kumgusa mwanamke ambaye haruhusiwi kwako.
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu