10. Waudumie watu vizuri wakati wa safari.
Sahl bin Sa’d (radhiyallahu anhu) anasema kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Kiongozi wa watu safarini ni yule anayewahudumia (yaani kiongozi awatumikie watu wake, au yule anayetumikia wengine aheshimiwe kama kiongozi, ingawa anaonekana kuwa mtumishi kwa kuwatumikia wengine). Yule anayewapita wengine kwa kuwatumikia watu, hawawezi kumzidi kwa kitendo chochote isipokuwa kupitia kupata kifo cha kishahidi (kwa sababu kwa kuwatumikia watu, ana sehemu katika kazi zote za haki wanazozifanya).
11. Usimsumbue mwenzako kwa njia yoyote ile wakati wa safari.
Abdullah bin Amr (radhiyallahu anhuma)anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Muislamu (mkamilifu) ni yule ambaye yuko salama kwa Waislamu wengine na madhara ya ulimi na mkono wake (yaani watu hawasumbuliwi kwa njia yoyote ile).
12. Unaposafiri katika kundi, mteue mtu mmoja kuwa ameer.
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Khudri (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Wanapotoka watu watatu safarini, basi wamchague mmoja wao kama amiri wa safari.”
13. Wakati wa kusafiri, ikiwa kikundi kitasimama mahali fulani kwa muda mfupi (k.m. kituo cha petroli) na nilazima uende kutekeleza baadhi ya haja au kujisaidia, basi wajulishe wenzako kabla hujaondoka.
14. Usijadili mada zenye utata au kuingia kwenye mabishano n.k na wenzio wakati wa safari.
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu