
Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) anataja kwamba siku moja alikuwa na baba yake kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) wakati Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akijadiliana na mtu kwa siri. Kwa vile Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akiongea na mtu huyo, mgongo wake ulielekezwa kwa Abbaas (Radhiya Allaahu ́anhuma) na mwanawe Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma), na pengine Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa hajatambuwa kwamba walikuwa wamekuja kukutana naye.
Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliondoka mbele ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na mwanawe na hakupata fursa ya kuzungumza na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).
Baada ya kuondoka, Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimwambia mtoto wake, Abdullah, “Ewe mwanangu! je uliona jinsi binam yako (akimaanisha mtume Sallallahu alaihi wasallam) ametugeuke (labda alikuwa hataki kuongea na mimi)?.
Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia baba yake: “Ewe baba yangu! Kulikuwa na mtu aliyekuwa pamoja na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ambaye alikuwa akiongea naye kwa siri (ndio maana Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) amekupa mgongo).
Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akataja: “Kisha tukarudi kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), na baba yangu alipokutana na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), akamwambia: “Ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)! Nilisema kadha na kadha kwa Abdullah (yaani. Niliwambia kuwa umetupa mgongo, na akanijulisha kwamba (sababu ya wewe kuniepusha ni kuwa) kuna mtu anazungumza nawe kwa siri (lakini sikuweza kumuona mtu huyo). Je, ni kweli kwamba ulikuwa unajadili jambo fulani kwa siri na mtu fulani?”
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alimuuliza Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu), “Ewe Abdullah! je ulimuona huyu mtu kweli (yaani yule mtu nilikuwa nazungumza naye)? Abdullah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Ndio (nilimuona)”.
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Mtu huyo (uliyemuona) ni Jibril (‘alayhis salaam) mtu ambaye nilikuwa nikizungumza naye.” (Musnad Ahmed #2679;Majmauz Zawaa’id #15518).
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu