Mtu mmoja alikuja kwa Zaid bin Thaabit (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuuliza kuhusu mas’alah ya dini. Zaid (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimpeleka kwa Abu Hurairah (Radhiyallahu ‘anhu).
Kisha Zaid (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia mtu huyo:
Wakati fulani nilikaa msikitini pamoja na Abu Hurairah na Sahaabi mwingine, huku nikishiriki katika dua na kumdhukuru Allah Ta’ala. Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuja na kuketi nasi. Kisha Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akatuambia: “Endeleeni katika yale mliyokuwa mkishughulika nayo (yaani. kufanya dua).”
Kwa hiyo mimi na swahabi mwengine tuliomba dua mbele ya Abu Hurairah, na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema amiin kwa dua zetu.
Baada ya hapo, Abu Hurairah alianza kuomba dua, ambapo akamuomba Allah Ta’ala ampe chochote tulichokuwa tumemuomba katika dua zetu. Pia aliomba dua ya kupewa elimu hiyo ambayo (itakaa naye milele na ambayo) hatoisahau.
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema Amin kwa Dua ya Abu Hurairah (Radhiya Allaahu ‘anhu). Zaid (Radhiya Allaahu ‘anhu) na swahabi mwengine waliposikia dua aliyoiomba Abu Hurairah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiomba apewe elimu hiyo ambayo hatoisahau kamwe, walimwambia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kwamba sisi pia tuombe dua ambayo Allah Ta’ala atatujaalia elimu ambayo hatutaisahau kamwe (yaani walitaka Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aseme Aamin kwenye dua zao).
Hata hivyo, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akawaambia: “Huyu kijana wa ukoo wa Daws (akimaanisha Abu Hurairah (Radhiya Allaahu ‘anhu)) amewapita nyinyi wawili (katika kuomba dua hii).”
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu