Wakati mmoja, wakati Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa safarini, Aaishah (Radhiyallahu anha) alininginiza pazia lenye picha za vitu vya uhai kwenye mlango.
Wakati huo, Aaishah (Radhiyallahu anha) hakuwa na habari kwamba picha za vitu vya uhai zimeharamishwa.
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alipofika nyumbani kwake na macho yake yakaangukia kwenye pazia, alichukizwa sana. Aaishah (Radhiyallahu anha) alimsalimia, lakini hakujibu salamu yake na mara moja akaliendea pazia na kulichana.
Kwa kuona mwitikio wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Aaishah (Radhiyallahu anha) alitambua kwamba alikuwa amefanya kosa kubwa, ambalo Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa amemkasirikia.
Kwa unyenyekevu wa hali ya juu na majuto, akasema, “Ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)! Ninarejea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa toba! Nielezee dhambi niliyoifanya.”
Moyo wa Aaishah (Radhiyallahu anha) ulijawa na mapenzi ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na Mtume Wake (sallallahu alaihi wasallam) kiasi kwamba haukuweza kustahimili kuudhika kwao hata dakika moja. Kwa hiyo, ingawa hakuwa na ujuzi wa dhambi aliyoifanya, kwanza aliharakisha kutubu na baada ya hapo akamuomba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amuelezee dhambi aliyoifanya ili asiirudie tena katika siku zijazo.
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kisha akamueleza matokeo mabaya ya wale waliohusika katika dhambi kubwa ya kutengeneza picha. Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Akasema: “Ewe Aaishah! Hakika watu wanaohusika katika kutengeneza picha za vitu vilivyo hai watapata adhabu kali zaidi Siku ya Qiyaamah.”
Ikumbukwe kwamba kama vile kutengeneza picha za vitu vilivyo hai ni haraam, hivyo hivyo kubaki na picha kama hizo pia hairuhusiwi. Jaabir (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikataza kuweka picha za vitu vilivyo hai ndani ya nyumba, na pia alikataza kutengeneza picha kama hizo.
Mtengeneza Picha Akipokea Adhabu Kali Zaidi Siku Ya Qiyaamah
Ukali wa dhambi ya kupiga picha unaweza kupimwa kutokana na Hadith ambayo Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ametaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa kwa adhabu kali siku ya Qiyaamah ni watu watatu wafuatao – mwenye kumuua Nabii au kuuawa na Nabii, kiongozi ambaye anawapoteza watu wake, na yule anayehusika katika utengenezaji wa picha za vitu vilivyo hai.
Hebu fikiria jinsi dhambi ya upigaji wa picha ni kubwa kiasi kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kamtaja mtengeneza picha pamoja na yule aliyemuua Nabii wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) au kiongozi wa taifa anayewapotosha watu wake!
Katika Hadith moja, imepokewa kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema kwamba kila mpiga picha atakuwa kwenye moto wa Jahannum. Katika Hadith nyingine, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Malaika (wa rehema) hawaingii kwenye nyumba ambayo ndani yake kuna picha (za vitu vilivyo hai).”

Kiumbe Ndani ya Jahannum Ambaye Atawaadhibu Watengenezaji wa Picha.
Katika Hadith ya Sunan Tirmidhi, imeandika kwamba Siku ya Qiyaamah, kichwa cha kiumbe kitaonekana kikitokea moto wa Jahannam. Kitakuwa na macho mawili ambayo yakuona, masikio mawili yakusikia, na ulimi yakuongea.
Itasema: “Nimeamrishwa kuadhibu makundi matatu ya watu; kila dhalimu anayeasi amri za Mwenyezi Mungu, na kila anayemuabudu yoyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na wale wanaojishughulisha na kutengeneza picha za vitu vilivyo hai.
Baada ya hapo, kiumbe huyo atawashika watu hawa na kuwatumbukiza ndani ya moto wa Jahannam.
Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Kutoingia Ndani ya Ka’bah kwa sababu ya Masanamu kuwa Ndani yake
Katika tukio la fathul Makka, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alitaka kuingia ndani ya Ka’bah, lakini alijizuia kuingia kutokana na masanamu kuwepo ndani ya Ka’bah.
Kwa hiyo, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliagiza kwanza masanamu yale yaondolewe ndani ya Ka’bah, na baada ya hapo akaingia ndani ya Ka’bah.
Baada ya kuingia ndani ya Ka’bah, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa ameona michoro ya vitu vya uhai kwenye ukuta za ndani za Ka’bah. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliwalaani wale waliohusika na kuchora picha hizi na baada ya hapo akaagiza kwamba michoro hii ifutwe.
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu