Maisha ya Nabii Isa (alayhis salaam) baada ya kurejea kwake na Baraka Kubwa na Usalama katika zama zake

Nabii Isa (‘alayhis salaam) atakaporejea duniani, Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atakuwa kiongozi anayewaongoza Waislamu. Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atamwambia Nabii Isa (‘alaihis salaam) kwamba awaongoze Waislamu, kwa sababu yeye ni Nabii wa Allah Ta‘ala.  (Ibnu Hibbaan #6812, Fitan li-Nu’aim #1028)

Wanajeshi ya Waislamu, chini ya uongozi wa Nabii Isa (‘alayhis salaam), watapigana vita na Dajjaal na kundi lake. Nabii Isa (‘alayhis salaam) atamuua Dajjaal na Waislamu watakuwa washindi katika vita hii.

Muda si mrefu baada ya hapo Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atafariki na Nabii Isa (‘Alayhis Salaam) ataswali janaazah. Nabii Isa (‘alayhis salaam) ataendelea kuishi katika ummah, akitekeleza sharia ya kiislamu na kuwaongoza watu kusilimu. Nabii Isa (‘alayhis salaam) ataowa na kupata watoto.

Baada ya muda kupita, Allah Ta’ala atawaachia Ya’juuj na Ma’juuj duniani. Watasababisha ufisadi na uharibifu duniani, popote waendako. Kisha Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) atawateremshia msiba utakaowafanya wote wafe.

Baada ya Ya’juuj na Ma’juuj kuangamizwa na Allah Ta‘ala, Allah Ta’ala atateremsha mvua nyingi, na kusababisha mimea kukua kwa wingi na wanyama kustawi. Watu wa dunia watabarikiwa kwa baraka kubwa sana wakati huo. Kutokana na baraka hii, ukubwa wa matunda na mazao pia utaongezeka. Pia kutakuwa na usalama kamili, kiasi kwamba watu hawatokuwa na hofu ya kudhuriwa na wanyama pori na wenye sumu kali. Mgawanyiko wa watu na ugumvi baina ya watu utakwisha pia kwa sababu uadui na chuki vitatoka kwenye mioyo ya watu.

About admin

Check Also

Kiwango cha Uadilifu na Kuridhika ndani ya Utawala wa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Katika baadhi ya hadithi, imeandikwa kwamba Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atatawala kwa uadilifu kiasi kwamba …