7. Soma Bismillah au dua ifuatayo kabla ya kula. Ikiwa upo na familia yako, basi unaweza kuisoma dua kwa sauti kuwakumbusha.
بِسْمِ اللهِ وَبَرَكَةِ اللهِ
Kwa jina la Allah (Ta’ala), na kwa baraka za Allah (Ta’ala).[1]
8. Wakati wa kula, ama kaa na magoti yote mawili juu ya ardhi (katika mkao wa Tashahhud), au kaa na goti la kulia likiinuliwa.
9. Kula na kunywa na mkono wa kulia.
Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Wakati mmoja wenu anakula au anakunywa, basi anapaswa kula kwa mkono wake wa kulia na kunywa kwa mkono wake wa kulia.”[2]
Sunna na Adabu Wakati Wa Kula
1. Mtu akisahau kusoma Dua kabla ya kula, basi anapaswa kusoma dua ifuatayo wakati mtu anakumbuka:
بِسْمِ اللهِ أَوَّلَهُ وَآخِرَهُ
(Ninaanza) kwa jina la Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) kwanzia mwanzo hadi mwisho.[3]
2. Wakati wa kula, ikiwa mkate wa chakula huanguka kwenye mkeka, basi uichukue, uisafishe na ule.
Jaabir (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Ikiwa mkate au chakula utaanguka (wakati unakula), basi anapaswa kuichukua, na kuisafisha na baadaye kula. Haupaswi kumuachia Shaitaan.”[4]
3. Usiegemee au kupumzikia chochote wakati wa kula.
Abu Juhaifah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Siegemeagi chochote wakati wa kula.[5]
[1] عن ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم وأبا بكر وعمر رضي الله عنهما أتوا بيت أبي أيوب فلما أكلوا وشبعوا قال النبي صلى الله عليه وسلم: خبز ولحم وتمر وبسر ورطب إذا أصبتم مثل هذا فضربتم بأيديكم فكلوا بسم الله وبركة الله (المستدرك للحاكم، الرقم: 7084، وقال: هذا حديث صحيح الإسناد ولم يخرجاه، وقال الذهبي: صحيح)
[2] سنن ابن ماجة، الرقم: 3266، وقال البوصري في مصباح الزجاجة 4/10 :هذا إسناد صحيح رجاله ثقات
[3] عن عائشة رضي الله عنها أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: إذا أكل أحدكم فليذكر اسم الله تعالى، فإن نسي أن يذكر اسم الله تعالى في أوله فليقل بسم الله أوله وآخره (سنن أبي داود، الرقم: 3767، مسند أبي يعلى، الرقم: 7153 ، وقال الهيثمي في مجمع الزوائد، الرقم: 7902: رجاله ثقات)
[4] صحيح مسلم، الرقم: ٢٠٣٣
[5] صحيح البخاري، الرقم: 5398