12. Ikiwa macho yako yanafunguka usiku, basi soma dua ifuatayo na baada ya hapo unaweza kumuomba Mwenyezi Mungu chochote. Insha-Allah, dua yako itakubaliwa.
لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرْ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ وَسُبْحَانَ اللهِ وَلَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَاللهُ أَكْبَرُ وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ اَللّٰهُمَّ اغْفِرْ لِيْ
Hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah (Ta’ala) Peke Yake. Hana mshirika. Ufalme ni wake Yeye tu, sifa njema zote ni zake, na Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, na hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi, na hakuna uwezo (kujiepusha na madhambi) na hakuna nguvu (ya kufanya vitendo vyema) isipokuwa kwa njia ya Mwenyezi Mungu. Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe!
Mtu anaweza pia kusoma dua ifuatayo:
لَا إِلٰهَ إِلَّا أَنْتَ سُبْحَانَكَ اللّٰهُمَّ أَسْتَغْفِرُكَ لِذَنْبِيْ وَأَسْأَلُكَ رَحْمَتَكَ اَللّٰهُمَّ زِدْنِيْ عِلْمًا وَلَا تُزِغْ قَلْبِيْ بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنِيْ وَهَبْ لِيْ مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنْتَ الْوَهَّابُ
Hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe! Umetakasika! ewe Mwenyezi Mungu! Nakuomba msamaha kwa dhambi zangu, na nakuomba rehma zako! Ewe Mwenyezi Mungu! Nizidishie elimu, wala usiuache moyo wangu upotee baada ya kuniongoza, na nibariki kutoka upande Wako rehma maalum, hakika Wewe peke yako ndiye Mpaji (wa baraka na fadhila zote)!
13. Usilale katika maeneo ambayo watu hutumia kama njia ya kupita (kama mlangoni) kwa sababu hii itawasumbua watu na inaweza kuwa njia ya wewe kuumia.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Wakati wa kusafiri kwenye malisho ya kijani vibichi basi mpe haki yake (kwa kusimama sehemu mbalimbali ili kumruhusu mnyama kuchunga malisho). Unaposafiri katika nchi kavu wakati wa ukame, basi kamilisha safari haraka (yaani usicheleweshe safari yako kwa kusimama mahali tofauti ili isiwe ngumu juu.
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu